HABARI NJEMA--TAASISI YA WAANDISI YAWAPA SOMO WANAFUNZI WA SEKONDARI YA TAMBAZA,SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
PICHANI NI SHULE YA SEKONDARI YA TAMBAZA PICHA NA MAKTABA |
Na Karoli
Vinsent
KATIKA
kuonyesha imedhamilia kuhakikisha
wanapatikana Waandisi bora nchini,Taasisi
ya Waandisi Nchini(Istitution of Engineer Tanzania IET) imewataka
wanafunzi kuacha kusomea masomo ya sanaa
peke yake badala yake wajikite zaidi kwenye masomo ya sayansi ili kulisaidia
Taifa liweze kupata waandisi wenye sifa,
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar
es Salaam na Rais wa Taasisi ya waandisi Tanania (IET) Injinia Dokta Malima
Bundala wakati alipokuwa anatoa elimu kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu
Waandisi katika Shule ya Sekondari Tambaza ambapo alisema ni wakati umefika wanafunzi
watanzania wakabadilisha mawazo na kuanza kuyapenda masomo ya Sayansi na
kuliokoa taifa , kutokana na kukosa kwake wataalumu wamasuala ya sayansi.
PICHANI KULIA NI Rais wa Taasisi ya waandisi Tanania (IET) Injinia Dokta Malima Bundala kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dokta magufuli akikabiziwa cheti picha na Maktaba |
“Taasisi ya waandisi nchini imeamua
kufanya shughuli za maendeleo na leo tumeanzia katika shule hii ya tambaza kwa
lengo la kuja shuleni hapa ni kutoa elimu kwa wanafunzi kuyapenda masomo ya
sayansi na kuliokoa taifa lilipo sasa kwa kukosa wataalamu mbalimbali wa
masuala ya sayansi ,kwani mambo haya ya uandisi ni mazuri katika kulisogeza
taifa lipige hatua”alisema Dokta Bundala,
Dokta
Bundala alizidi kusema wanafunzi wengi nchini wamekuwa waoga katika kusomea
mambo ya uandisi kwa kisingizio cha kukosa ajira lakini jibu ni hapana kwani
mambo ya Uandisi yanatoa uwanda mpana kwa mwanafunzi anapomaliza shahada yake na
kuweza kujiajiri,
Kwa upande wake Mwanafunzi wa Shule
hiyo ya Sekondali ya Tambaza Ratifa Juma aliipongeza taasisi ya Waandisi nchini
kwa elimu waliyoitoa kwani elimu hiyo imewafungua macho na kuanza kuyapenda
mambo ya Uandisi,
Naye mwanafunzi Mwengine wa shule
hiyo Bahati Wiliam John naye akisita kuipongeza Taasisi hiyo na kusema
imewafanya wafahamu vitu vingi ambavyo walikuwa hawavijui kuhusu mambo ya
uandisi na akaitaka Taasisi hiyo kuwa na utamaduni wakupita kila mara katika shuleni
hapo na shule zengine ili iwasaidie wanafunzi wengine wenye mawazo hasi kuhusu
mambo ya waandisi.
Huu ni Mwendelezo wa Shughuli za
Kijamii zinazofanywa na Taasisi hiyo kwani ilianza kufanya hivyo tangu
semptemba 21 mwaka huu na hadi tarehe 26 kwa kupita sehemu mbalimbali ikiwemo
shule pamoja sehemu zengine kwa lengo la kutoa elimu kwa Watanzania.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni