SIRI YA MAULIDI KITENGE KUHAMA RADIO ONE NA ITV HII HAPA,SABABU HIYO UWENDA IKAWAFANYA WATANGAZAJI WENGI KUHAMA REDIO ONE
Na Karoli
Vinsent
SABABU za
Mtangazaji Maarufu wa Kipindi cha Michezo na Burudani Maulidi Kitenge kuipiga Chini Radio one na Kuhamia Radio mpya E.fm 93.7 ya hapa Dar Es
Salaam, sasa sababu zaanza
kufichuka,Mtandao huu Umedokezwa Sababu hiyo.
Maulidi
Kitenge ambaye ametanga rasmi mwanzoni mwa wiki hii kupitia mtandao wake wakijamii wa facebook kwamba Miaka 14 aliyokaa
radio na Kituo cha Tv cha Itv inatosha yeye kukaa mjengoni hapo na tena yeye
kushindwa kuweka wazi sababu ya kuondoka hapo na kuondokea kwenye kituo kipya
cha Redio cha E.fm 93.7 Dar Es Salaam,
Taarifa za kuaminika Ambazo Mtandao huu
umedokezwa kutoka kwenye Vyanzo mbalimbali vilivyopo hapo E.FM Redio pamoja
na Radio one zinasema sababu iliyomfanya
aondoke hapo ndio sababu ambayo inahisiwa ndio itakayowafanya Watangazaji wengi waondoke
Radio one.
Akielezea
Sababu hiyo,Mfanyakazi wa kituo radio cha Efm, alichohaamia Kitenge ambaye
hakutaka Jina lake litajwe Mtandaoni alisema mtangazaji huyo amekosa uhuru ndio ikapelekea
kutoelewana na mabosi zake.
“Da ni kweli Kitenge sahivi ni
mfanyakazi Mwenzetu na teyali kasaini Mkataba,ila sababu iliyomfanya aondoke
pale Radio one,inatoka na y eye kuhusika katika kutengeneza Tangazo linalohusu Ujio wa Timu ya Wazee wa
Realmadrid ambao watakuja Tanzania wiki ijayo,sasa baada ya kutengeneza Tangazo
lile Viongozi Radio one wakakasirika kwa yeye kutengeneza Tangazo linalohusu
redio nyingine tena kwenye Studio tofauti na hapo”alisema mpashaji huyo
Chanzo hicho kilizidi kusema
mara baada ya kitenge kutengeneza Tangazo hilo aliitwa kujitetea na Mabosi wa Radio one,lakini yeye alionekana kama
anakosa Uhuru kutokana na kuingiliwa hata sehemu zengine ambazo hazihususiani
na kazi yake kutokana na kufanya kazi pale inapohitajika,ndipo akachukua
maamuzi ya kuachana Radio hiyo.
Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta
Mkurugenzi wa Radio One Deogratus Rweyunga na kutaka kujua ukweli wa taarifa
hizi,ambapo Rweyunga alimtaka Mwandishi wa Mtandao huu amtafute Kitenge
mwenyewe na kuzidi kusema yeye hana ugomvi na kitenge.
“Hebu sikiliza Mtafute Kitenge
mwenyewe,maana yeye kwenda kwenye Radio hiyo ni changamoto zengine na
tunamtakia maisha mema na sisi hatuna ugomvi na kitenge kaamua kuacha kazi hapa
ni sawa yeye ameona ni sahihi,na harafu unaposema Tangazo hilo alilotengeneza ndio
imetufanya tukasirike na tumfukuze kazi sio kweli kwani mbona yeye katengeneza
matangazo mengi ikiwemoa Tamasha la matumaini hatujakasilika na limepigwa Radio
nyingi sana na tumfukuza ili iweje leo ”alisema Rweyunga
Mwandishi wa Mtandao huu alipomtafuta kitenge
kujua ukweli wa Taarifa hizo hakuweza kupatikana mara moja kutokana na
kutopatikana kwenye simu,
Sababu hiyo ya kitenge Kuondoa Radio
one iliwai kutolewa mara kwa mara kwa
Watangazi waliohama hapo wakisema wanakosa
Uhuru wanapokuwa kwenye Radio hiyo.
2 comments
mwandishi wa blog hii tafadhali jifunze kiswahili fasaha UNA IAIBISHA TAALUMA YA UANDISHI yaani unashindwa kutofautisha L na R aibu yako....mfano umeandika "HATUJAKASILIKA"huo ni uchafu andika "HATUJAKASIRIKA" ukishindwa rudi shule kajifunze upya
Mimi nafikiri kila kazi ina mipaka yake, Sasa huyo mwandishi anaesema kuwa Maulid hakuwa na uhuru sijui uhuru huo ni upi sasa. Ni lazima tuheshima mipaka ya kazi. Wanahabari wengi wamekuwa wanagombanisha watu kwa kupekenyua habari ambazo wala hazipo. Sijui ndio staili yao ya kuuza magazeti. Acheni usaliti. Napendekeza ingeundwa mahakama ya ICC kwa ajili ya waandishi wa habari wanaochochea uhasama.
Post a Comment