Zinazobamba

SIRI YA MAULIDI KITENGE KUHAMA RADIO ONE NA ITV HII HAPA,SABABU HIYO UWENDA IKAWAFANYA WATANGAZAJI WENGI KUHAMA REDIO ONE



Pichani Kushoto ni Mkurugenzi wa Vipindi wa Radio Mpya E.fm 93.7 Dar es Salaam Diksoni ponela kulia ni Mtangazaji alikacha Radio Maulidi Kitenge na kujiunga Radio hiyo, akisaini Mkataba tayali kuanza kazi

Na Karoli Vinsent
SABABU za Mtangazaji Maarufu wa Kipindi cha Michezo na Burudani Maulidi Kitenge  kuipiga Chini Radio one  na Kuhamia Radio mpya E.fm 93.7 ya hapa Dar Es Salaam, sasa sababu  zaanza kufichuka,Mtandao huu Umedokezwa Sababu hiyo.
         Maulidi Kitenge ambaye ametanga rasmi mwanzoni mwa wiki hii kupitia mtandao wake  wakijamii wa facebook kwamba Miaka 14 aliyokaa radio na Kituo cha Tv cha Itv inatosha yeye kukaa mjengoni hapo na tena yeye kushindwa kuweka wazi sababu ya kuondoka hapo na kuondokea kwenye kituo kipya cha Redio cha E.fm 93.7 Dar Es Salaam,
              Taarifa za kuaminika Ambazo Mtandao huu umedokezwa kutoka kwenye Vyanzo mbalimbali vilivyopo hapo E.FM Redio pamoja na  Radio one zinasema sababu iliyomfanya aondoke hapo ndio sababu ambayo inahisiwa ndio  itakayowafanya Watangazaji wengi waondoke Radio one.

             Akielezea Sababu hiyo,Mfanyakazi wa kituo radio cha Efm, alichohaamia Kitenge ambaye hakutaka Jina lake litajwe Mtandaoni alisema  mtangazaji huyo amekosa uhuru ndio ikapelekea kutoelewana na mabosi zake.
          “Da ni kweli Kitenge sahivi ni mfanyakazi Mwenzetu na teyali kasaini Mkataba,ila sababu iliyomfanya aondoke pale Radio one,inatoka na y eye kuhusika katika kutengeneza Tangazo  linalohusu Ujio wa Timu ya Wazee wa Realmadrid ambao watakuja Tanzania wiki ijayo,sasa baada ya kutengeneza Tangazo lile Viongozi Radio one wakakasirika kwa yeye kutengeneza Tangazo linalohusu redio nyingine tena kwenye Studio tofauti na hapo”alisema mpashaji huyo
                Chanzo hicho kilizidi kusema mara baada ya kitenge kutengeneza Tangazo hilo aliitwa kujitetea na Mabosi  wa Radio one,lakini yeye alionekana kama anakosa Uhuru kutokana na kuingiliwa hata sehemu zengine ambazo hazihususiani na kazi yake kutokana na kufanya kazi pale inapohitajika,ndipo akachukua maamuzi ya kuachana Radio hiyo.
          Mwandishi wa Mtandao huu alimtafuta Mkurugenzi wa Radio One Deogratus Rweyunga na kutaka kujua ukweli wa taarifa hizi,ambapo Rweyunga alimtaka Mwandishi wa Mtandao huu amtafute Kitenge mwenyewe na kuzidi kusema yeye hana ugomvi na kitenge.
            “Hebu sikiliza Mtafute Kitenge mwenyewe,maana yeye kwenda kwenye Radio hiyo ni changamoto zengine na tunamtakia maisha mema na sisi hatuna ugomvi na kitenge kaamua kuacha kazi hapa ni sawa yeye ameona ni sahihi,na harafu unaposema Tangazo hilo alilotengeneza ndio imetufanya tukasirike na tumfukuze kazi sio kweli kwani mbona yeye katengeneza matangazo mengi ikiwemoa Tamasha la matumaini hatujakasilika na limepigwa Radio nyingi sana na tumfukuza ili iweje leo ”alisema Rweyunga
           Mwandishi wa Mtandao huu alipomtafuta kitenge kujua ukweli wa Taarifa hizo hakuweza kupatikana mara moja kutokana na kutopatikana kwenye simu,
        Sababu hiyo ya kitenge Kuondoa Radio one  iliwai kutolewa mara kwa mara kwa Watangazi waliohama hapo  wakisema wanakosa Uhuru wanapokuwa kwenye Radio hiyo.

2 comments

Anonymous said...

mwandishi wa blog hii tafadhali jifunze kiswahili fasaha UNA IAIBISHA TAALUMA YA UANDISHI yaani unashindwa kutofautisha L na R aibu yako....mfano umeandika "HATUJAKASILIKA"huo ni uchafu andika "HATUJAKASIRIKA" ukishindwa rudi shule kajifunze upya

Anonymous said...

Mimi nafikiri kila kazi ina mipaka yake, Sasa huyo mwandishi anaesema kuwa Maulid hakuwa na uhuru sijui uhuru huo ni upi sasa. Ni lazima tuheshima mipaka ya kazi. Wanahabari wengi wamekuwa wanagombanisha watu kwa kupekenyua habari ambazo wala hazipo. Sijui ndio staili yao ya kuuza magazeti. Acheni usaliti. Napendekeza ingeundwa mahakama ya ICC kwa ajili ya waandishi wa habari wanaochochea uhasama.