MAMALAKA YA ELIMU TEA YAUNGANISHA NGUVU NA WADAU KUSAIDIA KUONDOA TATIZO LA WANAFUNZI KUKETI CHINI, 156000000 ZATUMIKA KUNUNUA MADAWATI,
Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Sylvia Lupembe akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu jitihada wanazofanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu,wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji toka Mamlaka ya Elimu Tanzania, KCB, TOTAL, Social Action Trust Fund (SATF) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mipango waliyoiweka kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania katika kuendeleza na kuinua sekta ya Nchini.kushoto ni Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha Msuya.
Afisa Rasilimali Fedha toka taasisi isiyo ya kiserikali ya Social Action Trust Fund (SATF) Bw. Timotheo Tenga akiwaeleza jambo waandishi wa habari( hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha Msuya
Daresalaam,
Mamlaka ya elimu TEA kwa kushirikiana na makampuni ya ndani
ya nchi wametoa msaada wa madawati 2000 kwa shule 10 za jijini Darsalaam ikiwa
ni jitihada za kuondoa changamoto zinazowakabili wanafunzi wanaosoma katika
mazingira magumu
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, meneja
habari ,Elimu na mawasiliano wa mamlaka hiyo B. Silyvia Lupembe amesema msaada
huo unatarajiwa kunufaisha jumla ya wanafunzi 6000 katika shule 10 huku
jitihada zingine zikichukuliwa kuwafikia wanafunzi wengine wanaosoma wakiwa
wamekaa chini nje ya jiji la Daresaalam
Bi Lupembe alizitaja shule ambazo zinatarajiwa kunufaika na
udhamini huo wa madawati kuwa ni pamoja na shule ya msingi
Chamazi,Mbande,,Boko,,NHC,Hekima,Bwawani,Bunju, na Kingugi, Zingine ni shule ya
msingi Kombo,Goba,na King’ong’o
Bi Lupembe ametoa wito kwa makampunii mengine yenye nia ya
kusaidia katika sekta ya elimu kujitokeza na kuja kusaidia watoto wetu ambao
wanasoma katika mazingira magumu ambayo hayamruhusu kupata elimu iliyo bora
kutokana na miundo mbinu ya shule kutoruhusu kutoa elimu iliyo bora
Naye afisa mahusiano wa kampuni ya mafuta ya TOTOL ambao
wameanzisha mchakato huo wa kufadhili madawati kwa shule zenye uhitaji mkubwa,
Bi Masha Kileo amesema wazo la kuja kusaidia shule zilizo katika uhitaji mkubwa
wa madawati limekuja baada ya kuona wanafunzi wakisoma katika mazingira mabovu
huko shule za msingi,
Bi Kileo ameongeza kusema kuwa madawati hayo ambayo
yanatarajiwa kukabidhiwa kwake katika shule hizo za jijini Daresalaam
yameghalimu jumla ya shilingi million
156,000,000 ambazo zimechangiwa kwa pamoja na kampuni ya KCB bank, na mfuko wa
kusaidia jamii wa Social Action Trust Fund (SATF).
MAGARI…………………….PRESS…………………21.08.2014
No comments
Post a Comment