MRADI WA TRANS -SEC KUNUFAISHA WAKULIMA WADOWADOGO,PROF TUMBO TOKA SUA ASEMA HAIJAWAHI KUTOKEA,
| Ahadiel Mmbughu akifafa nua jambo katika mkutano huo |
Chuo cha Sokoine Sua kikishirikiana na Chuo cha Ujerumani , vinatarajiwa kuondoa tatizo la uhaba wa chakula cha uhakika katika maeneo ya walala hoi huko vijijini kufuataia kkuja na mradi mshirikishi uliolenga kuangalia mnyororo mzima wa thamani ya chakula ili kubaini changamoto zake na kuja na majawabu yatakayohakikisha chakula kinapatikana kwa wingi,
Akiutangaza mradi huo kwa wadau mbalimbali wakiwemo wakulima wenyewe, wamiliki wa viwanda, masoko, Mineja mradi toka Chuo cha kilimo Sua Prof. Siza Tumbo amesema mradi huo wa miaka mitano umelenga kuhakikisha uhakika wa chakula unaongezeka kwa asilimia kubwa huko vijijini,
Prof. Tumbo amesema, hali ilivyo sasa ni kwamba hakuna chakula cha uakika huko vijini na kwamba mradi umekuja katika wakati muafaka wa kuondoa changamoto ya kutopatikana kwa chakula cha uhakika,
| wadau katika mkutano huo wakifuatailia mada zinazowasilishwa na wataalam, |
Mradi huo unaotarajiwa kughalimu jumla ya ERO milion 7, unadaiwa kumkomboa mkulima mdogo kwani ni mradi unaoatarajiwa kuwashirikisha wakulima wengi katika hatua zake za uzalishaji,
Prof Tumbo amesema mradi huo utashirikisha jumla ya vijiji viwili toka katika mikoa miwili ya Dododma Na Morogoro ambapo katika vijiji hivyo jumla ya wakulima 150 kila kijiji wanatarajiwa kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo.
Katika hatua zake za kwanza, mradi umebaini baadhi ya changamoto zinazopelekea chakula cha uhakika kisipatikane nazo ni pamoja na sewrikali kushindwa kufikisha mbolea kwa wakati, kutoa kodi kubwa ya mazao changamoto ambazo zinawavunja nguvu wakulima kwa kiasi kikubwa
| Picha ya pamoja ya wadau hao waliokutana katika mkutano huo wa siku mbili uliofanyika huko ubungo jijini Daresalaam. |
No comments
Post a Comment