Zinazobamba

KUTEKETEA KWA MOTO MSIKITI WA MTAMBANI--DK SLAA ASONONEKA SANA.ATOA YA MOYONI SOMA HAPA KUJUA ALIYOYASEMA



 
Pichani ni Katibu Mkuu  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dk. Slaa atoa pole Msikiti wa Mtambani, ajionea athari .

            Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Slaa amefika Msikiti wa Mtambani kutoa pole kwa waumini na viongozi wa msikiti kwa niaba ya chama kutokana na tukio la moto lililotokea juzi jioni.

            Katibu Mkuu ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Chama Kanda ya Pwani, Prof. Abdalah Safari mbali ya kutoa pole pia alipata fursa ya kuzunguka maeneo mbalimbali kujionea madhara ya ya moto huo ambao hadi sasa kwa mujibu wa Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam unakadiriwa kusababisha uharibifu mkubwa wa mali zenye thamani ya Tshs. Mil. 600.

           Baada ya kuambiwa na Shehe Katimba mahitaji ya dharura kwa wakati huu, Dk. Slaa aliguswa na suala la wanafunzi wa Seminari ya Mvumoni kukosa vitu muhimu kwa ajili ya masomo yao hasa walioko Kidato cha Nne ambao wanajiandaa na mitihani yao ya kuhitimu, ambapo aliomba apewe tathmini ya mahitaji kwa wanafunzi hao ili chama kiweze kushirikiana na shule na wadau wengine kuwasaidia waendelee na masomo

1 comment

Anonymous said...

that's one of politics tricks he wants votes from muslims ndo mana anajifanya kuguswa sana na hilo jambo he is the enemy of Muslims and not helper refer to Surat tauba