HABARI NZITO LEO----JAJI WEREMA APINGANA NA IKULU YA RAIS KIKWETE,ASEMA BILA UKAWA HAKUNA KATIBA SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Mwanasheria Mkuu wa Tanzania Jaji Fredrick Werema akiwa na Mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila Picha na Maktaba.
Na Karoli
Vinsent
KILE
kinachoonekana Mchakato upatikanaji
katiba mpya umeanza kuwachanganya Viongozi wa Serikali ya Rais Jakaya
Kikwete,kutokana na wao kuanza kutofautiana kuhusu idadi ya theluthi 2 ya
wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mtandao huu unaripoti.
Mchanganyiko huo umegundulika leo
Jijini Dar es Salaam na Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredricki Werema
wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari alioutisha mahususi ili kuzungumzia
kuhusu mchakato wa katiba
Ambapo Werema alisema anahofu juu ya
uwezekano wa Katiba mpya kupatikana kutokana na kukosa theluthi 2 wajumbe
kutoka Zanzibar ambao wengi wao ndio waliogoma kurejea na kujiundia Umoja wa
kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA.
“Kuhusu Idadi ya kura za wajumbe wabunge
maalum la katiba inatoa wasiwasi kwasababu kwenye Kamati zile theluthi 2 ya
wajumbe inapatikana bila shida ila tatizo itakuja wakati wakupitisha Rasimu
iliyojadiliwa na Bunge ndio itatupa shinda kwasababu lazima ipatikane theruthi
ya 2 ya wajumbe wa Tanzania Bara na,”
“ Zanzibar sasa ungiangalia hapa kwa hali
ilivyo kama ikiendelea hivi bila ya kuwepo UKAWA itakuwa ni shida kupata
Theluthi 2 ya wajumbe kutoka kwa wajumbe wa Zanzibar na hapa ndio watu wanasema tutakuwa
tumetumia pesa nyingi sana za walipa kodi harafu hakuna katiba ndio maana
nawaomba ukawa warejee”alisema Werema.
Jaji
Werema ambaye naye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba alizidi kusema endepo hali hiyo ikitokea itabidi
Bunge la kawaida likae na kuanza kuifanyia marekebisho katiba ya sasa iliyopo
hususani kwenye vipengere vinavyopigiwa kelele ikiwemo kuwepo na tume huru ya
uchaguzi na sehemu zengine ili kuipa nafasi ya kutafuta Theruthi 2 kwa
wajumbe kutoka Zanzibar.
Kauli ya Mwanasheria mkuu wa
Serikali Jaji Werema inazidi kuwachanganya wananchi kutokana na Juzi Ikulu ya
Rais Jakaya Kikwete kusema Katiba mpya itapatikana hata kama Wajumbe wanaunda
Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA bila hata kuwepo kutokana na umoja huo kuwa
na idadi ndogo sana ya wajumbe.
Ikulu hiyo ilizidi kusema kuhusu
idadi iliyopo ya wajumbe kwenye Bunge Maalum la Katiba inatosha sana kuweza
kupata idadi ya Theruthi 2 ya wajumbe kuweza kuipigia kura vipengere hivyo.
Kauli hiyo pia ilitolewa na Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Samwel
Sitta ambapo alisema katiba mpya itapatikana bila ya UKAWA kuwepo,kwani Idadi
ya Wajumbe iliyopo inatosha sana kupata katiba mpya.
Kwa kauli ya Mwanasheria mkuu
Jaji Werema inakwenda sambamba na Mwanasheria wa Umoja wa Kutetea katiba ya
Wananchi UKAWA,Tundu Lissu ambapo naye aliuambia mtandao huu kwamba Ikulu ya
Rais Jakaya Kikwete inajisumbua kusema Idadi ya wajumbe wanatosha kupisha
rasimu inayojadiliwa na Bunge Maalum na kusema sio kweli,
Kwani idadi iliyopo Bungeni ni ndogo
kutokana na Sheria kusema lazima kuwepo na idadi ya 2 ya 3 kutoka kwa wajumbe.
Katika hatua Nyingine Mwanasheria wa
Serikali Jaji Werema aliwaomba Wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
UKAWA waliosusia bunge hilo kurejea kwenye bunge hilo kwani wao ni watu muhimu
sana .
“Mimi nawaomba ndugu zangu hawa wa Ukawa
warejee bungeni kwani mchakato huu unahitaji ushirikiano wao,hebu tuajiulize
sote tunaitaji mchango wa Tundu Lissu wakati wa kujadili masuala ya haki za
Binadamu tunataka kujua yeye anasemaje lakini kukataa kuja seheme zingine s,nawaomba
sana warudi jamani,wengine wajumbe hawa tunasali nao kanisani ikiwemo ndugu
yangu Mbatia aje bwana bungeni”alizidi kusema Werema.
Vilevile Jaji Werema alisema kwa
sasa Hakuna kipengere chochote cha Sheria kinachompa Mamlaka Rais Jakaya
Kikwete kulivunja Bung la Katiba na kuwataka watu wanasema hivyo waende kusoma
sheria.
No comments
Post a Comment