Zinazobamba

MAJANGA YAZIDI KUIKUMBA CLAUDS RADIO,SASA TCRA YAZIDI KUIKABA KOO RADIO HIYO SOMA HAPA KUJUA



 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj1usN5ShyiMFa6U6jG54I8hbY4GLJ-PlelC6_I6aYW_hgCVxY68bAKJ2AcLPrfxVI1gz7LLhwLiZTIWbJD8-BtsucFquoGxrCLXMl1Ds0Mx8Zds9y61Iql8Q8eq_Az5rQEQNfyzApROrU/s1600/SAM_0783.JPG
 Mwenyekiti wa kamati ya maudhui ya TCRA, Mhandisi Margaret Tabu Munyagi, akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari picha na Maktaba

Na Karoli Vinsent
MAJANGA yanazidi kuiandama kituo cha Radio cha Clauds Fm,baada ya leo Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA,kuipiga Faini ya Milioni Nane za kitanzania kutokana na kutangaza Kipindi kisichokuwa na maadili kwa watanzania.
     Kwa Mujibu wa Taarifa  iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kwenye vyombo vya habari na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya vipindi vya Radio nchini kutoka kwenye Mamlaka hiyo,Eng Margalet T Munyangi  inasema maamuzi hayo yamefikiwa kutokana na kuridhishwa na ushahidi waliokuwa nao,

        Ambapo Mamlaka hiyo inasema Faini hiyo inatokana na kituo hicho kukiuka sheria ya Utangazaji nchini ya mwaka 2005,kwa kuruhusu Kipindi cha Njia panda kilichorushwa tarehe 15-06-2014 kwaanzia saa 8.00 mchana hadi saa 10.00 jioni,katika kipindi hicho ilikuwa na mada ya Safari ya kuzimu,
          Mada hiyo ilikuwa ni ya kufikirika na kichawi zenye kudanganya umma ambao walikuwa wakisiliza kipindi hicho,kwani kufanya hivyo kituo hicho cha Radio kilikiuka sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 namba 5(a) (b) (c) (f) (g) (h) na 14 1 na 15 b ambapo kifungo hicho kinakataza Radio kutangaza vipindi visivyokuwa na Maadili.
        Aidha Mamlaka hiyo Imesema kituo hicho kimekiuka tena sheria hiyo ya Utangazaji  mwaka 2005 kifungu namba 22(1) ,(3) (a),(b) kwa kushindwa kutoa taarifa kwenye gazeti la kuhusu taarifa ya vipindi vyake kwa umma,ambapo sheria hiyo inavitaka vituo vyote vya Radio kutoa taarifa ya vipindi vyake kwenye Mamlaka hiyo pamoja na kwenye Gazeti lakini Clauds hawakufanya hivyo.
         Vilievile Mamlaka hiyo imesema baada ya kubaini makosa hayo kamati kuu ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini TCRA ilikaa na kuanza kuchukua ushahidi pamoja na kuwaita Wahusika wa Radio hiyo kuja kutoa utetezi wao,
             Ndipo Mkurugenzi  wa Radio hiyo Ruge Mtahaba aliitwa kuja kuto utetezi lakini naye  alikiri kosa kwa kuruhusu kipindi hicho na kushindwa kufanya usahihi wa Taarifa hiyo baada ya kugundua kuna makosa,
                Kutokana ushahidi huo Mamlaka hiyo imewapiga faini Radio hiyo ya Milioni Nane za kitanzania na kuitaka Radio hiyo ilipe pesa hizo ndani ya mwezi Mmoja kutoka siku ya uamuzi ambao ni leo.
                   Mamlaka hiyo imetoa rai kwa kituo hicho kutangaza kwa kutumia weredi na maadili kwani wakiendelea hivyo mamlaka hiyo haita wafumbia macho na kuzidi kusema itachukua hatua kali ikwemo hata kuwanyang’anya leseni.
              Huu ni Mwendelezo wa Majanga yanayozidi kuiyandama Clauds Radio kutoka na hivi sasa Radio hiyo kuingia Mgogoro na umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA  kutokana na Radio hiyo kusema haita soma  habari zinazohusu umoja huo kwa Madai umoja huo ni Wabinafsi.
         UKAWA ni muunganiko wa vyama vya Kisiasa ikiwemo Chadema,CUF,NCCR,mageuzi,NLD pamoja na wajumbe wengine 201 waliochaguliwa na Rais umoja huo umejiapiza kutorejea bungeni kwa madai Mwenyekiti wa Bunge hilo Samwel Sitta ameguza Bunge hilo kama mkutano wa chama chake cha CCM,

1 comment

Anonymous said...

kiswahili fasaha ni-:
kuiyandama -ni kuiandama
kwaanzia- ni kuanzia
weredi- ni weledi
na mengine nimeacha so post zako nimezipenda ila kiswahili unakivunja man..!!