Zinazobamba

HABARI NZITO--MCHUNGAJI MSIGWA AITETEA IKULU YA RAIS KIKWETE,AIBUKA NA KUYAVAA MAGAZETI NA KUTOA KAULI NZITO--SOMA HAPA KUJUA ZAIDI



Pichani Ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mchungaji Peter Msigwa akiwa jukwaani Picha na Maktaba.

Na Karoli Vinsent
SIKU chache kupita Baada ya Magazeti nchini kuituhumu ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kwa kutoa kibali maalum  kwa Familia ya Friedkin kutoka nchini Marekani ambao ni Marafiki wa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, kwa ajiri ya kuua Wanyama 704 ikiwemo Tembo pamoja na wanyama wengine.
       Naye Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii,Mchungaji Peter Msigwa ameibuka na kuyavaa magazeti nchini na kusema yanaandika Habari za Uongo.
        Kauli hiyo kushangaza ya Msigwa ameitoa leo Jijini Dar Es Salaam,wakati alipokuwa anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu,kuhusu Taarifa iliyoripotiwa na baadhi ya Magazeti juu ya Leseni iliyotolewa na ikulu kwa ajiri ya kuua wanyama 704,

         Ambapo msigwa alisema taarifa hizo sio za ukweli kwani ni za uzushi mtupu kutokana na Magazeti hayo kushindwa kuweka ushahidi wa moja kwa moja.
        “Sikiliza mwandishi mimi siwezi kuzungumzia vitu vinavyoandikwa kwenye gazeti la Fahamu,Raia Mwema pamoja na Jamhuri kwani tumeshayazoea kuandika habari za uzushi mtupu,na hiyo nakala ya barua wanayoitoa kwenye Gazeti sio ya ukweli tena inalengo ya kupotosha umma tu ndio maana kambi ya upinzania tumeipotezea”alisema Msigwa.
           Peter Msigwa ambaye ni mbunge wa Iringa Mjini CHADEMA alizidi kusema kawaida ni Vema taarifa hiyo ingekuwa na ushahidi kamili lakini wao hawakufanya hivyo na kuzidi kusema magazeti hayo yamekuwa yakipinga kile alichokifanya yeye ikiwemo kumshinikiza waziri wa maliasili na Utalii Lazaro nyalandu kuifungia leseni ya uwindaji,
Kwa Kampuni ya uwindaji ya Safari.
        “Mimi ningetegema magazeti hayo yangeiga mfano wa gazeti la Gurdian limekuwa likiandika makala ya kupongeza kwa kazi kubwa iliyofanywa ya kuifungia kampuni ya safari,kutokana na kitendo chake cha kufanya uwindaji haramu lakini cha kushangaza magazeti hayo yamebadilika yamekuwa yakiandika habari za uongo zenye kudanyanya Umma hizo taarifa hazina ukweli zinafedhehesha ikulu”alizidi kusema Msigwa.
     Mwandishi wa Mtandao huu alipomtajia Nakala ya barua kutoka ikulu ambayo magazeti hayo wanaitumia kama ushahidi ,Mchungaji Msigwa alimtaka Mwandishi wa Mtandao huu amtafute Waziri nyalandu atoe ufafanuzi kuhusu barua hiyo kutokana na  yeye kutoamini taarifa zinazoandikwa kwenye magazeti hayo.
“Mimi ningeshtuka kama taarifa ingeandikwa kwenye Gazeti la mwananchi,Tanzania Daima,Majira lakini unaniambia Taarifa kwenye Magazeti ya Fahamu,Jamhuri,Raia Mwema,wakati hawana ukweli kuhusu taarifa zao,na siwezi kuwazuia kwani wamekuwa wakibeza kazi nzuri ninayofanya mimi kwa kushirikiana na Waziri Nyalandu”
Kauli hiyo ya Mchungaji Msigwa inazidi kuchanganya Watanzania kutokana na Taarifa iliyolipotiwa na Magazeti nchi ambayo yamekuwa yakituhumu Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kuingia kwenye Mtego mchafu ulioandaliwa na Waziri wa Maliasili Lazaro nyalandu kutoa Leseni hiyo.
          Ambapo Leseni hiyo imetoa Ruhusa kwa  tembo wanane wameruhusiwa kuuawa nchini kwa kibali maalumu cha Rais (Presidential Hunting Licence).
         Kibali hicho kilichotiwa saini na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori aliyeteuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu baada ya kung’olewa katika nafasi hiyo Mkurugenzi wa awali, Profesa Jafar Kidegesho, kimetolewa rasmi Agosti Mosi, mwaka huu na mwisho wake wa matumizi ni kesho, Agosti 21, mwaka huu.
               Katika leseni hiyo ya Rais, watu wanane wa familia moja wameruhusiwa kuua tembo wanane kila mmoja, sambamba na wanyama wengine ambao jumla yao ni 704. Tembo wanane maana yake ni meno ya tembo 16.
         Kwa kawaida, presidential hunting license haitozwi malipo yoyote na hutolewa kwa malengo makuu matano. Lengo la kwanza ni kwa ajili ya shughuli za utafiti wa kisayansi; pili, ni kwa ajili ya shughuli za maonyesho katika makumbusho (museum); tatu ni kwa ajili ya masuala ya elimu; nne, kwa ajili ya shughuli za kiutamaduni na tano kwa ajili ya uwindaji ili kupata chakula pale inapojitokeza dharura ya njaa.
           Hata hivyo, kinyume cha vigezo hivyo vitano, leseni hiyo ya uwindaji ya Rais inayoruhusu kuwinda wanyama 704, imetolewa kwa familia ya Kimarekani ya Friedkin, taifa ambalo limepiga marufuku biashara ya meno ya tembo.
                Katika leseni hiyo ya Rais, kila mwanafamilia anaruhusiwa kuwinda jumla ya wanyama 88 kutokana na aina (species) 49 tofauti bila kulipa chochote kwa sababu ya hadhi ya leseni husika.