HABARI NJEMA MDA HUU---RITA YAZINDUA MFUMO THABITI WENYE LENGO BORA KWA WATANZANIA--SOMA HAPA KUJA ZAIDI
| Pichani katikati Afisa Mtendaji mkuu na Msajili Mkuu,wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Philip G,Saliboko Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam,(picha na Exaudi Mtei) |
Na Karoli Vinsent
WAKALA wa
Usajili na ufilisi na Udhamini(RITA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu(NBS) inatarajia kufanya tasmini ya mfumo wa Usajili,matukio muhimu ya
Maisha na ukusanyaji wa Takwimu nchini.
| Waandishi wa Habari kutoka Vyombo tofauti tofauti wakisikiliza kwa makini |
Akizungumzia Tasmini hiyo, leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi Habari ,Afisa Mtendaji mkuu na Msajili Mkuu,wakala wa Usajili Ufilisi na
Udhamini (RITA) Philip G,Saliboko Alisema Tasmini hiyo itafanyika kianda kwa
siku kumi na tano
(15) kuanzia tarehe 15 Semptemba hadi tarehe 30 mwaka huu na
itajumuisha wadau wakubwa wa Masula ya usajili kutoka wizara ,Taasisi,Idara
pamoja na Vyuo na wakala Mbalimbali za Serikali.
Ambapo aliongeza kusema Tathmini
itafanywa katika ofisi za Maafisa tawala wa Wilaya,Vituo vya Tiba ,Vituo vya
Polisi,nyumba vya kutunzia Maiti,makanisa na kwenye Makazi ya Wananchi ambamo
matuko hayo utokea.
Saliboko aliwataka Watanzania
kutoa ushirikiana mkubwa wakati wa Zoezi hili,kwani ndio njia pekee
itakayoisaidia Serikali kufanya mipango yake kikaminifu.
No comments
Post a Comment