Zinazobamba

UKAWA WALIPASUA TAIFA,SASA WAMNYIMA USINGIZI RAIS KIKWETE,SOMA HAPA UONE JINSI TAIFA WALIVYOLIPASUA TAIFA



                 UKAWA wamsaka JK 

KATIKA kusaka suluhu ya kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba, wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wanakusudia kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili kumtaka atafute ufumbuzi wa suala hilo kwa sababu ndiye alivuruga mchakata huo.
        Hatua hiyo inakuja baada ya UKAWA kupuuza juhudi za maridhiano zilizoanza kufanywa na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, wakidai hawana uamuzi.
         Wiki hii, Sitta alitangaza kuitisha kikao cha maridhiano Julai 24, ambacho kitawashirikisha pia viongozi kadhaa wa dini, lakini UKAWA wanahoji uhalali na dhamira ya mwenyekiti huyo; ikiwa alishindwa kulimudu Bunge anawezaje kutafuta muafaka nje?

                  Tanzania Daima limedokezwa kuwa katika mwendeleo wa Serikali ya CCM kuhaha kunusuru mchakato huo, Jaji Mutungi naye alifanya kikao na viongozi wa UKAWA na CCM jijini Dar es Salaam akitaka pande hizo zijadiliane namna ya kurudi Bunge la Katiba.
         “Msajili alitaka kila upande uandike kueleza tatizo lililopo na kifanyike nini ili tuweze kurudi kuendelea na Bunge la Katiba litakaloanza mwezi ujao,” kilisema chanzo chetu.
             Kwa mujibu wa chanzo hicho, katika mazungumzo hayo, yalijitokeza mambo mawili, moja likiwa ni uhalali wa Bunge la Katiba kuwa na mamlaka ya kuifumua na kuibadili rasimu ya katiba na pili ni mamlaka ya msajili kuitisha kikao hicho akidhani atapata suluhu wakati hana uamuzi.
       “Sisi tuliandika mapendekezo yetu kwamba kwa kuzingatia sheria ya mabadiliko ya katiba, Bunge Maalum halina mamlaka ya kuifumua rasimu na kuibadilisha bali kuiboresha.
         “Sheria imetoa madaraka kwa tume ya kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu, Bunge la Katiba kazi yetu ni kuboresha rasimu na mwisho wananchi watapiga kura ya kuipitisha au kuikataa katiba,” alisema mtoa habari wetu.
        Kwamba katika mazungumzo hayo, ulizuka mvutano mkali kati ya pande hizo kwani wakati UKAWA wakishikilia msimamo kuwa kazi ya Bunge la Katiba ni kuboresha rasimu, CCM wanatetea kwamba wajumbe wa Bunge hili wanaweza kufanya chochote katika rasimu.
       Katika hoja ya pili kuhusu uhalali wa msajili kuitisha kikao hicho kutafuta suluhu, UKAWA wanasema aliyepaswa kufanya hivyo ni mwenye mamlaka, yaani Rais Kikwete aliyeasisi mchakato huo.
        “UKAWA tunamtaka rais mwenyewe tuzungumze naye, tumweleze kuwa alilikoroga yeye kwa kuvuruga mchakato, hivyo atafute suluhu. Lakini CCM hawataki maana hawamwini kila anapokutana na sisi katika hili.
         “Msajili hawezi kutafuta muafaka wa hili, hana maamuzi. Tumekubaliana kukutana tena Julai 21 mwaka huu, baada ya kuwa amepitia hoja zetu, lakini baada ya hapo tutakwenda kwa rais,” alisema.
        UKAWA wanasisitiza kuwa Rais Kikwete amekuwa msikivu kila wanapokutana naye kuzungumzia mkwamo wowote katika mchakato wa katiba mpya, ingawa tatizo liko kwa chama chake.
Sitta
          Kuhusu kikao cha maridhiano alichokiitisha Sitta, Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu, aliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa amekurupuka pasipokujua anachokifanya.
          Lissu alisema kuwa Kamati ya Maridhiano ipo kikanuni za Bunge hilo ambalo Sitta alishindwa kulimudu hadi UKAWA wakalisusia na hivyo kuhoji hao wajumbe wa kamati hiyo wakiwemo viongozi wa dini anaodai amewaweka amewatoa wapi?
          Alisema kuwa Sitta anazunguka kuhadaa wananchi, kwamba anatafuta muafaka wakati alishiriki kuvunja kanuni za Bunge Maalum la Katiba na sasa anawanyooshea vidole UKAWA.
Chanzo ni Gazeti makini la Tanzania Daima.

Hakuna maoni