MCH.MSIGWA AMLIPUA TENA KOMBORA JINGINE MALIASILI NA UTALII,AIBUKA NA KUWAPONDA WAANDISHA WA HABARI,SOMA HAPA UJUE ALICHOKISEMA
Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mchungaji Peter Msigwa.picha na Maktaba
Na Karoli
Vinsent.
SIKU chache
kupita baada Waziri wa Maliasili,Lazaro Nyalandu kuifutia Leseni ya Uwindaji
Kampuni Green Miles Safari Limited(GMS) kutokana na kuendeleza vitendo vya
kutesa wanyama pamoja na kuvunja sheria za Uwindaji,
Naye,Waziri
Kivuli wa Maliasili na Utalii,Mchungaji Peter Msigwa,ameibuka na kumtaka Waziri
Nyalandu kupitia Upya Kampuni zote za Uwindaji hapa nchini kwani nazo zimekuwa
zikifanya kazi kinyume na sheria.
Kauli hiyo
ya Msigwa ameitoa Mda huu wakati alipokuwa anafanyiwa Mahojiano na Mwandishi wa
Mtandao huu kwa Njia ya Simu kutoka Iringa,
Ambapo Mwandishi wa Mtandao huu
alitaka kujua anachukuliaje Hatua iliyochukuliwa na Waziri nyalandukufungia
kampuni hiyo ya Uwindaji.
Ndipo,
Msigwa alisema ni mda umefika kwa Waziri Nyalandu kupita upya kampuni
zinazofanya Uwindaji hapa nchini kwani zimekuwa zikifanya kazi kinyume na
taratibu.
“Katika hili
nampongeza kwa kuchuka Hatua,cha msingi namtaka asiishie kwenye Kampuni
hii,inabidi kuyachukulia makumpuni mengine ya uwindaji, tena inabidi achunguze
kwa makini kampuni zengine ambazo zimekuwa zinafanya ubabaishaji kwenye
uwindaji hapa nchini”alisema Msigwa
Mchungaji
Msigwa,ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini CHADEMA,alimpongeza Waziri Nyalandu kwa
kitendo chake cha kutoa itikadi zake za Chama na kuweka Maslahi ya Taifa mbele
kwani suala la Uwindaji haramu linapaswa kupigwa vita na kila mtu mpenda
maendeleo katika Taifa hili.
Katika Hatua
nyingine Mwandishi wa Mtandao huu alipomtaka atoe ufafanuzi kuhusu Taarifa
zinazoandikwa kwenye Magazeti mbalimbali hapa nchini .
Kwamba
kitendo chake cha kupinga kampuni hii iliyofungiwa ya Uwindaji Kampuni Green Miles Safari
Limited(GMS) inatokana na Yeye kufanya Njama ili Kampuni ya Wengbert Windrose
Safari (WWS)inayomilikiwa na Wamarekani ipiwe kitalu hicho cha Uwindaji
kilichipo Ziwa Natrion?
Msigwa
alijibu kwa Hasira alisema anashindwa kuwaelewa Waandishi wa Habari wa nchi
hii, kushindwa kujibu hoja ya yeye aliyoibua kuhusu unyama huo unaofanya na
Kampuni hiyo uwindaji Green Miles Safari Limited(GMS).
“Mimi
ningetegemea Mwandishi makini wa Habari angeibuka nakupinga ushahidi ule na
kujibu hoja kwamba niliyosema yana uongo au la kwamba Wanyama wale hawa
ulipigwi,lakini kusema kwamba mimi naipendelea kampuni hiyo sio za Kweli”
“Kwahiyo
kama wao wanaugomvi na Kampuni nyingine mimi hayanihusu,mimi hapa nazungumzia
ukiukaji wa haki na kwamba kama ipo kampuni nyingine ikifanya kinyume na
taratibu mimi nakufa nayo”alisema Msigwa.
Mwandishi wa
Mtandao huu alipotaka kujua kama hatayachukulia hatua zozote za kisheria
Magazeti haya ambayo yamekuwa yakimshutumu kwamba amehongwa na kampuni hiyo ya Wengbert
Windrose Safari (WWS)inayomilikiwa na Wamarekani ?
Mchungaji,Msigwa
ambaye ni Mwanasiasa Machachali kutoka Chadema alisema Hawezi kubishana na Watu
waliokosa maana, yeye anakazi nyingi za kufanya.
“Mwandishi
kuna kazi nyingi sana za kufanya siwezi nikabishana na watu wasiojielewa kwani mtu akiandika kama mimi ni mwanamke harafu eti
mimi nianze kubishana na mtu aliyeandika hivyo wakati mimi ni mwanaume,mimi nawaacha waandike
najua wataacha”
“Mimi kukaa
na Wajinga ambao wanatumiwa na watu binashfi ili waweze kukwamisha kasi yangu
ya kulinda wanyama pori hapa nchini”alisema Msigwa.
Mchungaji Msigwa
ndiye mtu waliyeibua hujuma inayofwanywa na Kampuni uwindaji Green Miles Safari
Limited(GMS) kupitia mkanda wa Video ambapo msigwa alisema Kampuni hiyo imekuwa
ikifanya uwindaji kinyume na taratibu.
Ndipo,jitihada
hizo za Mchungaji Msigwa zilimuibua Waziri wa Maliasili,Lazaro Nyalandu,na
kuifutia Leseni kampuni hiyo,
Akisoma maazimia hayo jana mbele ya Waandishi wa Habari waziri Nyalandu alitaja makosa hayo kuwa ni wageni wa kampuni hiyo kuwinda wanyama ambao hawakuruhusiwa kwenye leseni ya uwindaji wakiwemo nyani na ndege, jambo ambalo ni kinyume na kifungu cha 19(1)(2).
Pili, wageni wa kampuni hiyo kuchezea watoto wa pundamilia na ngiri kinyume na kifungu cha (19)(1), wageni kufukuza wanyamapori kwa magari na kisha kuwapiga risasi wakiwa ndani ya magari kinyume na kifungu 65(1) (a) 1, kuwinda wanyama walio chini ya umri (watoto), kinyume na kifungu cha 56(1).
“Kuruhusu watoto chini ya miaka 16 kuwinda kinyume na kifungu cha 43(2) (a), na wageni kuwinda huku wakipiga kelele, jambo ambalo ni kero kwa wanyama na kinyume na kifungu cha 19(1) na (2),” alisema.
Nyalandu alikiri kampuni hiyo kuvunja sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009, sambamba na kanuni za uwindaji, na kwamba kwa kuzingatia mamlaka aliyopewa chini ya sheria hiyo ya kuhifadhi wanyamapori No.5, amechukua hatua.
“Kwa kuzingatia matakwa ya kanuni ya 17(1), 8(2), nafuta umiliki wa vitalu vyote vilivyo chini ya Kampuni ya Green Miles Safaris Ltd, hii ikiwa ni pamoja na vitalu vya Lake Natron GC East, Gonabis/ Kidunda-WMA na MKI-Selous.
“Pia, hatua hii inafuta vibali vyote vya uwindaji vilivyotolewa katika msimu huu wa uwindaji na hii iwe onyo kwa kampuni za uwindaji wa kitalii nchini kuhusu ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za uwindaji,” alisema.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni