JOPO LA WAHARIRI LATEMBELEA MIRADI YA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU WA NHC MTANDA, LINDI NA SHANGANI MTWARA
Juzi,
Alhamisi (Julai 10, 2014) na jana Ijumaa (Julai 11, 2014) jopo la Jukwaa
la wahariri takriban 85 walitembelea kwenye miradi yetu miwili, mmoja
wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu Mtanda mkoani Lindi na mwingine wa
nyumba za makazi za kati na juu zilizopo eneo la Shangani Mtwara.
Jopo hilo
likiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Absalom Kibanda na Katibu wa
Jukwaa hilo, Neville Meena. Walisomewa taarifa fupi ya maendeleo ya
ujenzi wa miradi ya Nyumba hizo zipatazo 30 Lindi ambazo sasa zimefikia
kwenye hatua za mwisho tayari kwa kukabidhiwa kwa wamiliki wake kwani
nyumba zote 30 tayari zilishanunuliwa na zile za Mtwara ambazo pia ni
30, 10 kati ya hizo zikiwa zimeshanunuliwa.
Miongoni
mwa mambo makubwa yaliyozungumzwa na wahariri hao ni kuliomba kuendelea
kusimamia azam yake ya kuwauzia nyumba Watanzania wa kipato cha chini,
kwani kwa kufanya hivyo watanzania wa kawaida watakuwa na uwezo wa
kumiliki nyumba na siyo kuendelea kuwa wapangaji wa shirika.
Wahariri wakifuatilia maelezo ya Meneja wa mkoa wa Mtwara wa Shirika la Nyumba la Taifa, Joseph John (hayupo pichani) wakati Meneja huyo akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa mradi huo jana mbele ya Wahariri.
Wahariri
wakifuatilia maelezo ya Meneja wa mkoa wa Mtwara wa Shirika la Nyumba
la Taifa, Joseph John (hayupo pichani) wakati Meneja huyo akitoa taarifa
fupi ya utekelezaji wa mradi huo jana mbele ya Wahariri.
Wahariri
wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Meneja wa Shirika
la Nyumba Mtwara, Joseph John walipotembelea mradi wa nyumba za makazi
za Shangani Mjini Mtwara jana jioni. Kutoka kulia ni Jabir Idrisa,
Mhariri wa Mwanahalisi, Salim Salim nguli wa Habari na Mwalimu kutoka
Zanzibar, Joseph Kulangwa wa Uhuru Publications.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni