UKAWA NI BALAA,RAIS KIKWETE AKUBALI YAISHE AANZA KUWAITA IKULU NA KUWABEMBELEZA ,SOMA HAPA UONE JINSI ILIVYO

HUJUMA
aliyoifanya Rais Jakaya Kikwete kwenye mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya
na kupelekea Wajumbe wanaounda umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA
kususia vikao vya Bunge la Katiba ,sasa hali hiyo yaanza kumtesa Rais Kikwete
Mtandao umebaini.
Vyanzo
vya Uhakika kutoka ndani ya chama cha
Mapinduzi CCM, zinasema chama hicho kinafikilia kuukubali muundo wa Serikali
tatu ambao unatokana na Rasimu ya maoni ya wananchi,kuachana na Rasimu ya kipropaganda
ya chama hicho inayozungumzia muundo wa
Serikili mbili.
Chama hicho kikongwe kulichopo kusini
mwa jangwa la Sahara ambacho kipo madarakani,kimeamua kulegeza kamba na kufuata
maoni ya wananchi kutokana na kupata shinikizo kubwa kutoka kwenye Madhehebu ya
Dini nchini pamoja msimamo mkali uliowekwa na Muungano wa Kutetea Katiba ya
Wananchi,UKAWA.
Licha ya Rais Jakaya Kikwete,kutumia
kila njia ili wajumbe kutoka UKAWA,kurudi kwenye bunge la Katiba,kwenye vikao vyake
vinavyotarajiwa kuendelea tena mwezi ujao,kugonga mwamba baada ya kumtumia
msajili wa vyama vya kisiasa nchini Jaji Francis Mutungi,ambaye ameonekana
kushindwa kazi hiyo ya kuwashawishi warudi kwenye bunge hilo lilokuwa likibedha
maoni wananchi.
Kwa mujibu wa mjumbe wa kamati kuu ya CC
kutoka CCM,anasema”kwa hali iliyopo kwa sasa hakuna jinsi lazima tukubali muundo
wa serikali tatu ambao umetokana na maoni ya wananchi,kwani tumemshauri
mwenyekiti wetu Rais Kikwete, akubaliane na hawa wajumbe wa UKAWA,kwani serikali tatu ndio kila kitu”alisema mjumbe
huyo wa juu kamati ya chama cha mapinduzi ya ccm.
Mwandishi wa mtandao huu
amedokezwa,Rais Jakaya Kikwete teyali ameipiga chini kauli yake aliyoitoa
wakati wa ufunguzi wa Vikao vya Bunge la Katiba,ambayo alitoa maelekezo kwa
wajumbe wa Bunge hilo wakubaliane na muundo wa Serikali tatu na kupiga chini
maoni ya Wananchi.
Ambapo Rais Jakaya Kikwete teyali
amekutana Faragha na wajumbe wanaunda Umoja wa katiba ya Wananchi UKAWA,ikulu
jijini Dar Es Salaam ili kupata mwafaka juu ya kukwamua mchakato wa katiba
ambao aliuvuruga mwenyewe.
Chanzo hicho kilisema Mkutano kati ya
Rais kikwete na Mjumbe mwandamizi wa UKAWA,mkutano huo ulifanyika usiku wa wiki
iliyopita kutokana na ombi la Rais .wito wa Rais Kikwete kwa UKAWA ulifanyika
kwa njia ya Simu.
Kuhaha huku kwa Rais Kikwete kuukwamua
mchakato huu kumekuja baada siku mbili
tangu Halmashauri kuu ya 48 bya jumuiya ya kikristo Tanzania (CCT)iliyokutana
tarehe 2 na 3 mwaka huu ,kuelekeza waumini wake kupigania kuwepo serikali tatu ambayo
inapingwa vikali na CCM,
Duru za Kisiasa zinasema mwenye
uwezo wa kukwamua mchakato huu wa katiba ni Rais Jakaya Kikwete ambaye ndio aliuhalibu
mwenyewe,licha ya Jitihada alizofanya mwenyekiti wa Bunge la katiba, waziri
Sitta kutumia nguvu zake zote kuwasii wajumbe hao wa UKAWA wanaotetea maoni ya
Wananchi kurudi Bungeni.
Teyali wajumbe hao wa UKAWA wakiwa
wametoa sharti moja tu ili wajumbe hao waweze kurudi kwenye vikao vya bunge la
katiba ni kwa Wajumbe wa chama cha Mapinduzi CCM,kuacha kujadili Rasimu ya kwao
badala yake wajadili Rasimu iliyotokana na Maoni ya wananchi.ambacho sharti
hilo limekuwa ngumu sana kwa chama hicho kubaliana na hali hiyo.
Duru hizo zilisema kama Rais Jakaya Kikwete
akishindwa kukwamua mchakato huu wa Katiba basi atakuwa amejihalibia katika Nyanja
mbalimbali za Siasa nchini,endapo akiondoka madarakani mwakani mwezi wa kumi,na
kujijengea sifa mbaya ya kiongozi aliyepelekea nchi kupoteza mabilioni ya fedha
kwenye mchakato wa katiba ambao alihuharibu mwenyewe kwa kauli zake.
No comments
Post a Comment