WAFUASI WA CCM,CHADEMA NUSURA WAZITWANGE
Mbunge
wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (KULIA), akiamulia ugomvi wa
Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa
CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea
mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla
katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo,
Dar es Salaam jana.
Wafuasi
wa CCM na Chadema wakitaka kuzipiga kavu kavu baada ya kutokea mzozo
ambapo wanaCCM walikuwa wakimzomea Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John
Mnyika akihutubia na WanaChadema wakimzomea Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla akihutubia katika mkutano huo.
Poilisi wakiwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipinga Mbunge wao John Mnyika asijibu swali lililoulizwa na Mkazi wa Kibamba, Jordan Balindo aliyemtaka Mnyika aeleze ni jitihada gani amezifanya binafsi kama mbunge kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika jimbo la Ubungo.
Mfuasi wa CCM akiwa na bango la kumshutumu Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka, Dar es Salaam, EvaSinare (katikati) akijaribu kuunusuru mzozo huo kwa kuzungumza na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mfuasi wa Chadema akiwa na bango la kuishutumu Serikali
Polisi akilinda usalama mbele ya mashabiki wa CCM na Chadema
Mbunge wa Jimbola Kinondoni, Idd Azzan akihutubia katika mkutano huo
Wafuasi wanawake wa CCM na Chadema wakichimbia mkwara
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia kwakueleza utekelezaji wa Ilani
ya CCM, ambapo aliwahakikishia wananchi wa jiji la Dares Salaam kwamba
ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao tatizo la maji litakuwa historia hasa
baada ya kukamilika upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu ambao ujenzi
wake umeanza sasa.
Makalla akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi kuhusu ujenzi wa Tanki jipya la maji eneo la Kibamba, Dares Salaam,wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dares Salaam na Pwani.
Mkazi wa Kibamba, Chrisant Kibogoyo akiuliza swalikatika mkutanouliofanyika Kata ya Kibamba.
Mwalimu
wa Shule ya Msingi ya Kibwegere, Hellen Mshana akiuliza swali kwa waziri
kwambanilini maji yatasambazwa katika shule hiyo na zinginezo
Askari akimuondoa mfuasi wa Chadema aliyekuwa akilazimisha kumuuliza swali Waziri Makalla katika mkutano huo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Maji Safi na Taka Dares Salaam, (Dawasco),
Jackson Midalla akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa na Diwani wa Kata
ya Kibamba, Issa Mtemvu wakati Waziri Makalla, alipotembelea mradi wa
maji katika kata hiyo.
Wafuasi wa CCM na Chadema wakishindana kupeperusha bendera za vyama vyao wakiwakwenye magari eneo la Kibamba. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Hakuna maoni
Chapisha Maoni