Zinazobamba

MGANGA WA JADI AWAVUA NGUO ZOTE WANAWAKE ZA WATU KISHA KUWACHEZEA, ADAI NI DAWA YA KUPENDWA NA WAPENZI WAO .....

 
 Ama kweli uswazi hakuishi vijimambo! Mganga wa jadi almaarufu sangoma aliyetajwa kwa jina la Wadebi Jinasa amepata aibu ya karne baada ya kunaswa ‘live’ na wake za watu kwenye gesti moja (jina linahifadhiwa) iliyopo Tandika jijini Dar es Salaam.

Mganga wa jadi almaarufu sangoma aliyetajwa kwa jina la Wadebi akijutia baada yakunaswa live.
 Tukio hilo la aina yake lilijiri maeneo hayo, usiku wa manane wa kuamkia Jumanne iliyopita, wakati waumini wa Dini ya Kiislamu waliofunga kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakila daku.
Kwa mujibu wa mashuhuda, jamaa huyo alidaiwa kuwa alikuwa akiwafanyia wake hao wa watu dawa ya mapenzi kwa kuwavua nguo zote kisha ‘kuwachezea’.

Sangoma amekuwa akiwavuta wanawake wengi kwa kuwatajia matatizo yao sawia bila kukosea.
 Ilidaiwa kuwa mbali na kuwachezea, amekuwa akiwafanyia mchezo usiofaa mmoja baada ya mwingine.Chanzo cha sakata hilo kilidai kuwa sangoma huyo amekuwa na tabia hiyo hasa akimuona mwanamke mwenye mvuto katika hali ambayo haikueleweka mara moja humuita majina yake matatu, yaani la kwake, baba hadi la babu yake, jambo linalosababisha anayeitwa kushtuka na kuhisi mtu huyo atakuwa anamfahamu kiundani. 
Ilidaiwa kuwa baada ya mwanamke huyo kusimama huanza kumwelezea matatizo yake na kumtajiwa hadi matatizo yanayowapata ndugu zake walio vijijini na sehemu nyingine za mbali. 

Kiliendelea kudai kwamba, sangoma huyo amekuwa akiwavuta wanawake wengi kwa kuwatajia matatizo yao sawia bila kukosea hivyo kuwachanganya na kumjengea imani kuwa ni ‘fundi’ wa masuala hayo.
 Kufuatia vituko vyake, juzikati mume wa mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa), Huruka Hassan alirejea nyumbani kwake na kukuta mkewe hayupo.Alidai alipofanya uchunguzi wa haraka, aligundua ameenda kwenye gesti hiyo kupata tiba.
 Ilidaiwa kwamba, siku zote Huruka amekuwa akimuacha mkewe akapate tiba lakini siku ya tukio machale yalimcheza, alipofika kwenye gesti hiyo alijibanza ukumbini na kusikia sauti ya mkewe ikinong'ona chumbani na sauti ya 'besi' la sangoma huyo kwa mbaaali.
 Ilisemekana kwamba uzalendo ulimshinda Huruka na kujikuta akivunja masharti ya kilinge cha sangoma huyo kwa kuchungulia kwenye tundu la kupitisha funguo."Haaamadi!" alisikika Huruka alimuona laivu mkewe akiwa mtupu akitaka kufanyiwa vitendo vichafu ambapo sangoma huyo alidaiwa kuwa alikuwa akjiandaa kumfanyia ‘amshaamsha’.
 Ilidaiwa kuwa Huruka alishindwa kujizuia, akagonga mlango kwa hasira ambapo sangoma alivaa 'chapchap' na kufungua.Ilielezwa kwamba walipokutana uso kwa uso, Huruka alitunishiana misuli na sangoma huyo wakataka kuzichapa lakini jamaa akaona amchukue mkewe na kutimka naye. 

Baada ya mke wa Huruka kuokolewa kufanyiwa ukenge, mwanamke mwingine wa eneo hilo, Tabu Abdallah naye alidai kumnasa mkewe kwenye gesti hiyo akiwa amekalishwa kama alivyozaliwa, akitolewa vitu fulani tumboni na sangoma huyo. 

Akizungumza na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publisher ambayo ilifika eneo hilo usiku baada ya kutonywa na chanzo chake, Tabu alisema alimnasa mkewe na sangoma huyo baada ya kutonywa juu ya mkewe kuingia gesti hiyo. 
Alisema sangoma huyo alimchukua mkewe kwa gia ya kumtibia kumbe alikuwa na lake jambo.

Baada ya kutokea kwa mtiti huo, Mjumbe wa Shina namba 29, Azimio-Tandika, Faraj Neto, wanawake waliodhalilishwa, waume zao, polisi na mmliki wa gesti hiyo, Ebenezer Ngowo, walimchomoa sangoma huyo kwenye gesti hiyo. 

Katika hali ya kushangaza mke wa Tabu alikuwa akimlaumu mumewe kwa kutaka kumpiga mganga wake ambaye alikuwa akitaka kummalizia matatizo huku wanawake wengine wakiwaomba radhi waume zao na kudai walirubuniwa. 
Akizungumizia mkasa huo mke wa Tabu alisema kuna siku alikutana na mganga huyo njiani ambapo alimwita majina yake matatu, aliposimama kumsikiliza ndiyo akaanza kumtajia matatizo yake, jina la mama yake mzazi na kumwambia mama huyo huko aliko ana tatizo sugu la miguu jambo ambalo ni kweli ndipo alianza kumuamini. 

MWISHO WA SAKATA

Mwisho wa sakata hilo, mjumbe wa nyumba kumi alimtaka sangoma huyo kuondoka eneo hilo na mmiliki wa gesti hiyo alimtaka mganga  huyo kuhama kwenye gesti yake kutokana na tabia yake ya kubadilisha wanawake. 

Kwa upande wao, polisi walimshikilia sangoma huyo kutokana na sababu za kiusalama kufuatia wenye wake na wananchi wenye hasira kutaka kumpiga mawe na kumuua.

Hakuna maoni