TAARIFA KAMILI YA JESHI LA POLISI KWA WANANCHI KUHUSU SAKATA LA VIUNGO VYA BINADAM VILIVYOTUPWA JIJINI DARESALAAM HII HAPA
Jeshi la polisi kanda maalum sasa linawashikilia jumla ya watu wanane wakiwepo wafanyakazi wa taasisi ya IMTU wakihusishwa na sakata la utupwaji wa viungo vya Binadadam huko katika eneo la Bunju katika jiji la Draesalaam, kwa habari zaidi soma taarifa ya jeshi hilo hapa chini.
![]() | ||||
| Kamishina wa polisi kanda maalum ya Daresalaam akitoa ufafanuzi juu ya viungo vya binadam vilitupwa hapa jijini Daresalaam, Kamata kova amesema taarifa za awali zinaonyesha viungo hivyo vimetoka katika hospitali na chuo Cha IMTU hata hivyo jeshi hilo limeunda tume kuchunguza habari hiyo ili kubaini kwa nini viungo hivyo vya binadam kutupwa eneo hilo, |
![]() |
| Mabaki ya miili iliyotupwa eneo la Bunju Dar es Salaam |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
22/07/2014
WATU WANANE WAKIWEMO MADAKTARI WASHIKILIWA NA KUHOJIWA
NA JESHI LA POLISI KUTOKANA NA KUTUPWA VIUNGO VYA BINADAMU MAENEO YA BONDE LA MBWENI
MPIJI ENEO LA BUNJU
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia
watu wanane na kuwahoji kuhusu tukio la kupatina na viungo vya binadamu
vilivyogundulika katika maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji ambapo mifuko ya
plastiki ipatayo 85 yenye mabaki ya viungo vya binadamu yaligundulika. Polisi walipata taarifa 21/07/2014 jioni
kutoka kwa wasamaria wema na ndipo jopo la wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa
Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ACP. Camilius Wambura walifika hapo majira ya
saa 1.00 usiku.
Walipofika
katika tukio waligundua mifuko ipatayo 85 mieusi yenye viungo vya aina mbali
mbali vya binadamu kama vile Vichwa,
Miguu, Mikono, Mioyo, mapafu,
vifua na mifupa ya aina mbali mbali ya binadamu. Viungo hivyo havikuwa na uvundo au harufu ya aina
yoyote na vilionekana kwamba vimekaushwa na kukakamaa. Katika eneo hilo pia
vilikutwa vifaa vinavyotumika hospitali kama vile mipira ya kuvaa mikononi (gloves)
mifuko miwili iliyotumika ,nguo maalum (apron) zipatazo 20 na karatasi mbili
zenye maswali ya kujibu.
Wananchi
wasiopungua 1,000 walifika katika eneo hilo la tukio lakini hakuna aliyekuwa na
taarifa sahihi. Viungo hivyo
vilichukuliwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi. Aidha jopo la Wapelelezi chini ya Mkuu wa
Upelelezi Kanda Maalum ACP. Japhari Mohamed walianza uchunguzi mara moja kwa
kusaidiana na Daktari wa Jeshi la Polisi anayehusika na uchunguzi wa miili ya
binadamu (Forensic Doctor) ambaye kwa pamoja walishirikiana na madaktari
wengine kutoka hospitali wa Taifa Muhimbili.
Hatimaye
uchunguzi wa kina ulibaini kwamba viungo hivyo kwa mara ya mwisho vilikuwa
katika Maabara ya Chuo Kikuu Madaktari IMTU jijini D’Salaam. Baada ya kugundulika hivyo Polisi wamewakamata
na sasa wanaendelea kuwahoji watu wanane ambao wanasadikiwa kuhusika na miili
hiyo ikiwa ni pamoja na baadhi ya
madaktari wa IMTU. IMTU (International Medical and Technolegical
Univester) ni chuo Kikuu cha Madaktari ambacho pia hufanya mafunzo ya udakitari
kwa vitendo (practical). Jeshi la Polisi
Kanda Maalum litamuhusisha Mkemia Mkuu wa Serikali na hatimaye mara baada ya
kukamilika kwa uchunguzi jalada litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kwa hatua zake ili sheria ichukue mkondo wake.
S. H. KOVA
KAMISHNA WA
POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM


No comments
Post a Comment