Zinazobamba

KATIBU MKUU TAMISEMI AWAJIBU WANAOBEZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA, ASEMA HAYO NI MATUNDA YA BRN

Katibu mkuu wa TAMISEMI akifafanua jambo mbelel ya waandishi wahabari kuhusu upangaji wa nafasi za masomo kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka huu, ambapo katika upangaji huo jumla ya wanafunzi 54058 wamefanikiwa kupata nafasi huku wengine wakiahidiwa kufikiriwa kwa chaguo la pili ,
Katibu mkuu wa wizara ya tawala za mikoa  na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. Jumanne Sagini amewajia juu watanzania wachache ambao wamekuwa wakihusisha matokeo ya kidado cha sita kuwa ni matokeo ambayo yamepikwa ili kuonyesha kuwa mpango wa BIG RESULT NOW uonekane umefanikiwa, na kusema kuwa wanaofikiria hivyo wamekosea kwani matunda hayo yamechangiwa na nguvu nyingi za wanafunzi na walimu wao pamoja na watendaji katka sekta ya elimu kwa hivi sasa


Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo wakati anatangaza upangaji wa nafasi za wanafunzi waliojiunga na kidato cha tano mwaka huu, Sagini amesema kuna watu wameonekana kuwa hawaaminiamini kuhusu matokeo ya kidato cha sita, wanajiuliza ni kwa nini ufaulu umekuwa mzuri, jibu ni moja kuwa serikalini kwa sasa tumejipanga vizuri na ndio maana matunda yanaanza kuonekana kwa idai kubwa ya wanafunzi ambao wamejiunga na mafunzo kwa kidato cha sita kufaulu kwa wastani mzuri.

Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa karibu hutuba ya katibu mkuu wa TAMISEMI hii leo.

No comments