Pichani ni Kamanda wa kanda Maalum ya Dar Es Salaam kamishna Suleiman Kova akizungumza wandishi wa Habari mda huu,kuhusu viungo vya bindamu vilivyopatikana huko mbweni.
Na karoli Vinsent
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar
es Salaam limewatoa Hofu wakazi wa Jiji hili,na kusema viungo vya binaadamu
vilivyogundulika katika maeneo ya Mbweni Mpiji ni Vimetoka kwenye Chuo Kikuu cha
Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (International
Medical and Technological University – IMTU,ambapo vilikuwa vikitumika katika kujifunzia na sio Maeneo
mengine.
Hofu hiyo, imetolewa Mda huu na Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam, Suleman Kova wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari ambapo Alisema kuwa, Jeshi la polisi lilipokea
taarifa 21 Julai mwaka huu, majira ya jioni kutoa kwa wasamaria wema na ndipo
jopo la wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ACP
Camilius Wambura kufika maeneo hayo majiura ya jioni.
“Katika hatua za awali baada ya kufika
eneo la tukio waligundua mifuko 85 mieusi yenye viungo vya aina mbalimbali vya
binaadamu kama vile Vichwa, Miguu, Mikono, Mioyo, Mapafu, Vifua na Mifupa ya
aina mbalimbali ya binaadamu”
Alieleza kuwa, katika hali
iliyoshangaza kuwa viungo hivyo havikuwa na uvundo wala haraufu ya aina yoyote
na vilionekana kwamba vimekaushwa na kukakamaa.
“Katika eneo hilo pia vilikutwa vifaa vinavyotumikaa
hospitalini kama vile mipira ya kuvaa mikononi (gloves) mifuko miwili
iliyotumika, nguo maalum (apron) zipatazo 20 na karatasi mbili zenye maswali ya
kujibu”
Alisema kuwa licha ya eneo la tukio
kuwepo wananchi waasiopungua 1000 lakini hakuna aliyekuwa na taarifa
saahihi juu yaa sakata hilo.
“Viungo viliweza kuchukuliwa na
kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kufanyiwa uchunguzi, chini
ya Jopo la Wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda ya Maalum ACP
Japhari Mohamed akisaidiana na Daktari wa Jeshi la Polisi anayehusika na miili
ya binaadamu” alisema.
Kamishna Kova alieleza kwamba, baada
ya uchunguzi wa kina kufanyika ilibainika kwamba viungo hivyo kwa mara ya
mwisho vilikuwa katika Maabara ya IMTU jijini Dar es Salaam.
Katika hali nyingine isiyokuwa ya
kawaida Kamishna Kova alisema, wananchi wa eneo hilo waliopata taarifa waliamua
kulishikilia gari ndogo aina ya Canter ambalo lilikuwa limebebaa uchafu
uliokuwa unatoa harufu kali na kulihisi kuwa limebeba mifuko mingine ilkiyokuwa
na miili ya binaadamu.
“Gari hilo lilibainika wazi kwamba
halikuhusika na tukio hilo, pia tulipolipekewa ikagundulika limebeba mabaki ya
kuku ikiwemo Utumbo, miguu, vichwa na manyoya pamoja na uchafu mwingine
uliokuwa umeoza” alisema.
Katika kuhakikisha unapatikana
ushahidi wa kina Kamishna Kova alibahinisha kuwa Jeshi la Polisi litamuhusisha
Mkemia Mkuu wa Serikali na baada ya kukamilika kwa uchunguzi jalaada
litaapelekwa kwa Mwaanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zake ili sheria
ichukue mkondo wake.
|
No comments
Post a Comment