EXCLUSIVE---SAKATA LA KUFUNGIWA GAZETI LA MWANAHALISI SEHEMU YA KWANZA,
Pichani Ni Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Halihalisi Publishers Ltd Saed Kubenea ambo ni wachapishaji wa Gazeti la Mwanahalisi akiyaonesha magazeti yaliyosababishwa kufungiwa picha na Maktaba
Na Karoli
Vinsent
KATIKA
kujali ubora wa Gazeti la Mwanahalisi mtandao huu,unakuleta simulizi kuhusu
sakata la kufungiwa Gazeti hilo,ambapo gazeti hilo limefungiwa kwa mda
usiojulikana na Serikali kutokana na Habari zake zilizokuwa zikiandikwa ambapo kwa sasa limetinatiza miaka miwili.
Gazeti la mwanahalisi lilifungiwa
Tarehe 30/07/2012 na Waziri wa Habari ,vijana
utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ambapo
alitoa Hukumu ya kulifungia kwa muda usiojulikana kwa kile alichokiita kwamba
mwenendo wa Gazeti hilo si mzuri,kwani limekuwa likiandika Makala zenye
uchochezi na kuleta Uhasama na uzushi na
kupelekea wananchi kukosa Imani na Vyombo vya Dola hali inayoweza kuhatalisha
Amani ya nchi.
Ambapo, waziri huyo
alitumia Sheria Kandamizi ya Magazeti ya Mwaka 1976,kifungu Namba,25 ambayo
inampa Mamlaka waziri anae husika na masuala ya Habari, kulifungia Gazeti
lolote pale yeye mwenyewe anaona kwa mawazo yake kwamba Gazeti linakiuka sheria
ya nchi.
Adhabu hiyo ilianza kutumika
kwanzia Tarehe 30 mwezi Julai mwaka 2012,ambapo katika adhabu hiyo ilisema
kwanzia sasa gazeti hilo limefungiwa kwa mda usiojulikana.
Kwa sasa Gazeti hilo
limetimiza Miaka miwili tangu lifungiwe lakini bado hakuna nia ya dhati kutoka
kwa Serikali katika kulegeza Adhabu hiyo kubwa kwenye historia ya Magazeti
nchini, huku serikali ikijua kwamba Nchi yetu Tanzania iko kwenye ,Mfumo wa
Kidemokrasia ambao unatoa mwanya kwa Mtu kujieleza,
Vilevile Serikali imeshindwa hata kutambua kwamba ndani ya Katiba ya nchi
Ibara ya 18 ambayo inatoa uhuru wa
kujieleza kwa kila mtu.
Mtandao huu utakuletea
Mikingano ambayo imeibuka baada ya Gazeti hilo kufungiwa kutoka Kwa
Viongozi,ambapo malamala kwa mala wamekuwa wakitofautiana kuhusu kufungiwa gazeti
hilo ambalo lilibeba Taswira ya ukombozi katika fani hii ya Habari.
Gazeti la Mwanahalisi
lilianzishwa miaka mitano iliyopita na
kuwa chini ya Kampuni ya Halihalisi Publishers Ltd,ambapo mkurugenzi wa Kampuni
hiyo alikuwa ni Saed Kubenea.
Vilevile Kubenea ambaye ni miongoni mwa
Waandishi bora wanofanya Habari za uchunguzi nchini,ambaye alikuwa anafuata
nyayo za Mwandishi wa Zamani Gazeti la Mfanyakazi Stani Katabalo,ambaye naye
alikuwa ni Miongoni mwa Waandishi wanaofanya na Kuandika Habari za Uchunguzi
nchini katika kipindi hiko cha nyuma.
Licha ya Kubenea kuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Halihalisi
pia alikuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo la Mwanahalisi.
Katika Kazi za Hatari ni za
kufanya Habari za Uchunguzi Saed Kubenea aliwai kukumbana na Matatizo ikiwemo
kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikana na kupelekea kwenda kutibiwa nje ya
nchi ili kuweza kuoka Macho yake ambayo yalidhulika kwa Tindi kali hiyo aliyokuwa
amemwagiwa Usoni hususani kwenye Macho.
Lakini mpaka sasa Jeshi
la Polisi alijawai kuwataja wala kuwakamata watu waliohusika na kumfanyia
Vitendo hivyo vya kinyama mwandishi huyo nguli katika fani ya Habari nchini.
Gazeti hilo ambalo lilikuwa lilikuwa likifichua mambo ya mabaya
yaliyokuwa yakifanywa na Serikali,wanasiasa pamoja Viongozi wa Mashirika
mbalimbali hapa nchini,
Hii ni sehemu ya kwanza
ya Sakata la kufungiwa Gazeti hili la mwanahalisi,usikose tena kesho kujua
mengine kuhusu gazeti hilo,ambapo Mtandao huu utakuletea Simulizi ndefu kwanzia
leo tarehe 21hadi tarehe 25 mwezi siku ambayo ndio tarehe ya mwisho kuchapisha
Gazeti,Nia yetu ni tunataka umma ujue na kufahamu ukweli ulioko kwenye
Sakata la Gazeti hili na Sababu iliyopeleka kufungiwa Gazeti hili,
Tunafanya hivi labda
serikali yetu inaweza kubadilisha mawazo na kuweza kulifungulia Gazeti hilo
ambalo lilikuwa limetoa ajira kwa watanzania wengi hapa nchini.
No comments
Post a Comment