TAARIFA KAMILI YA SERIKALI KWA WANANCHI WAKE KUHUSU UTAPELI UNAOFANYWA NA WATU MITANDAONI WAKIJIDAI WANATOA MIKOPO YA FEDHA KUMBE NI MATAPELI WA KUTUPWA, SOMA HAPA
TAARIFA KAMILI HII HAPA
Napenda
kuwafahamisha wananchi kujihadhari na utapeli unaofanywa na baadhi ya taasisi
hewa hapa nchini zinazodai kutoa mikopo kwa wananchi kwa njia ya simu za
mikononi.
Katika miezi ya
hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la Taasisi hewa za fedha zinazotoa huduma
kwa njia ya mitandao ya simu za mikononi na kuwaadaa wananchi kwa kutumia
majina ya viongozi wa serikali, viongozi wa siasa na taasisi kubwa za kibenki.
Taasisi hizo pia
uweka namba za uongo za usajili kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
kuwagilibu wananchi kuwa taasisi hizo ni halali.
Mathalan, taasisi
inayojiita Social credit Loans inayoeleza
kuwa imesajiliwa TRA kwa namba Reg.
No.33/SCC/REG/REG/7894 na namba ya utambulisho
ya mlipa kodi TIN: 203-344-6789.
Ufuatiliaji
uliofanywa na TRA umebaini kuwa hakuna taarifa zozote kuhusu taasisi hiyo.
Taasisi nyingine
ni Saving Foundation na Quicken Loan.
Utendaji wa
taasisi hizi hutegemea mitandao ya simu za mikononi, mfano;
-Kupokea fedha za
waliojaza fomu zinazopatikana katika tovuti zao, na
-Kutuma mikopo.
Nambari
wanazotumia ni 0715 373 307, 0755 066
858, 0752 567 717 na 0654 441 494.
Pia napenda
kuwakumbusha wananchi wote kwa ujumla wakiwemo watumishi wa umma kutokubali
maombi ya fedha, fadhila au maelekezo yanayodaiwa kutolewa na uongozi wa juu bila
kupata uthibitisho kutoka mamlaka husika.
No comments
Post a Comment