EXCLUSIVE---MIAKA MIWILI YA KUFUNGIWA GAZETI LA MWANAHALISI---SEHEMU YA TATU,SOMA UJUE JINSI SERIKALI ILIVYOKULUPUKA KULIFUNGIA GAZETI HILO
Na karoli
Vinsent
BADO mtandao
huu unaendelea na Simulizi endelevu Juu
ya kufungiwa kwa Gazeti la Mwanahalisi,ambapo mtandao huu unafanya hivi ili
kwenda sawa na Tarehe ambayo gazeti hili lilifungiwa na Serikali kwa mda
usiojulikana,Gazeti la mwanahalisi ifikapo tarehe 25 mwezi wa saba mwaka huu
linatimiza Miaka miwili tangu lifungiwe na serikali.
Ambapo Gazeti hili lilifungiwa rasmi
tarehe 25 mwezi wa 7 mwaka 2012,kutokana na kuandika habari zinazodaiwa ni za
kichochezi,
Leo ni siku ya tatu ambapo bado
mtandao huu,unazidi kuendelea na simulizi hiyo,ambapo Jana tuliiweka habari
iliyopeleka kufungiwa kwa Gazeti hilo,Habari yenyewe ilikuwa inamzungumzia
Sakata nzima la linalomuhusu mwenyekiti wa Chama cha Madaktari nchini Dk Stevin
Ulimboka ambaye Gazeti hilo liandika juu ya mtu waliombaini kwamba anahusika
kumfanyia unyama Dokta huyo.
Baada ya kuandika habari hiyo
kwenye toleo namba 304,likamfanya Waziri wa Habari,utamaduni na Michezo
kulifungia Gazeti hilo,katika Tamko lake kwenye Vyombo vya Habari,ambapo
alisema amelifungia Gazeti hilo kwa mda usiojulikana na kusema Gazeti hilo
limekuwa likiandika Habari za Uchochezi pamoja kuleta Uhasama kati ya vyombo
vya Dola pamoja na wananchi,
Katika Tamko hilo lilosainiwa na
msajili wa Magazeti nchini,alisema kutokana na Sheria ya magazeti ya Mwaka 197o
kifungu cha 25,ambacho kimempa mamlaka ya kulifungia Gazeti,
Ambapo alizidi kusema Mhariri wa
Gazeti hilo ameitwa mara kwa mara na Wizara yake ili aweze kutoa Ushahidi au
kutoa ufafanuzi juu ya anachokiandika na Mhariri huyo alijitetea na kusema
katiba ya Nchi ibara ya 18 inampa mamlaka kutoa maoni.
Usikose tena kuendelea kusoma
mwendelezo wa Makala hizo zinazozungumzia kufungiwa kwa Gazeti la
Mwanahalisi,amabapo uchambuzi huu umekuja ikiwa ikenzi miaka miwili Tangu gazeti
hilo la mwanahalisi ,ambapo gazeti hilo,Tarehe 25 mwezi huu linatimiza miaki
miwili,
Na kesho
mtandao huu utakuja na Jinsi wanasiasa pamoja na Wanaharakati walipoibuka na
kupingana na Adhabu hiyo iliyotolewa kwenye gazeti hilo
No comments
Post a Comment