Zinazobamba

SAKATA LA UFISADI AKAUNTI YA ESCROW----LAFIKIA PATAMU,SASA KATIBU WIZARA YA NISHARTI NA MADINI AZIDI KUUMBUKA,SOMA HAPA UONE JINSI ANAVYOUMBUKA



 Pichani ni Katibu Mkuu Wizara ya Nisharti na Madini
Eliachim Maswi picha na Maktaba

Na Karoli Vinsent
HUKU kukiwa Bado Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikimfungulia kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi)  ikitaka ailipe sh. bilioni 310 kama fidia ya kuwachafulia jina kampuni hiyo.
        Vilevile  kampuni hiyo imewasilisha maombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ikitaka itoe zuio la muda kwa Kafulila asiendelee kuikashifu hadi shauri la msingi litakaposikilizwa.
        Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nisharti na Madini Eliachim Maswi,anazidi kuumbuka baada ya Nyaraka za Barua alizoiandika kuidhinisha pesa kutoka kuzidi kuvuja.

        Kashfa hiyo ya Ufisadi,ambayo haijawai kutoa tangu,tupate Uhuru, inawahusisha Waziri wa Nisharti na Madini Sospeter Muhongo, katibu wake  Maswi, Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanza nia, Prof. Ndulu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba kuwa walishiriki kuchota fedha hizo ambazo ni Zaidi  sh. bilioni 200 ,
        Fedha,hizo zimechotwa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow,licha ya Kafulila kutoa ushahidi wa Ufisadi huo, Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wake, Eliachim Maswi,  wamekuwa wakisisitiza kwamba fedha hizo zilitolewa kwa kuzingatia hukumu ya Mahakama Kuu.
     Mwandishi wa Mtandao huu,alishudia Barua hiyo iliyoandikwa Kupitia barua kumb. No. SAB.88/417/01/5 ya Oktoba 21, 2013, Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Maswi alimwandikia Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Benno Ndulu akimtaka aruhusu fedha hizo katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
        Katika barua hiyo, Maswi anakumbushia barua ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yenye Kumb. No. AGC/E.80/6/65 ya Oktoba 2, 2013 ambayo pia nakala yake ilikwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servaciaus Likwelile.
        Katika barua tajwa, AG anasisitiza umuhimu wa kutekeleza hukumu ya Mahakama Kuu bila kuchelewa, ikijumuisha pia na kumaliza mgogoro wa fedha za Akaunti ya Escrow,” inasomea sehemu ya barua hiyo na kuhitimisha kwamba;
         “Kwa barua hii, nakuomba kama wakala wa Escrow kuhamisha fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow kwenda IPTL kwa kuzingatia makubaliano kati ya Wizara ya Nishati na Madini na IPTL ya Oktoba 21, 2013.”
         Nakala ya barua hiyo pia ilipelekwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, Mwanasheria Mkuu, Jaji Werema na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Likwelile.
        Akaunti ya Tegeta Escrow ilifunguliwa kutokana na kuwapo kutoelewana kuhusu gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na IPTL na kuuzwa kwa Tanesco.
         Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID) katika uamuzi wake wa Februari 2014, ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco walitozwa kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL.
         Kwa uamuzi huo, ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadiwa kwenye akaunti hiyo maalumu ya Escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali.
  Habari hii imesaidiwa kwa kiwango kidogo na Gazeti Makini la Tanzania Daima

No comments