ABDULRAHMAN KINANA LAWAMANI, AHUSISHWA NA MIPANGO YA KUKWAMISHA UKAWA WASIONANE NA RAIS KIKWETE KUTAFUTA MWAFAKA SOMA HAPA KUJUA KWANINI,
Pichani ni KATIBU mkuu
wa Chama cha Mapinduzi CCM, Abdulrahman Kinana picha na Maktaba
Na Karoli
Vinsent
KATIBU mkuu
wa Chama cha Mapinduzi CCM, Abdulrahman Kinana Ametajwa kuwa ni
mtu anayekwamisha kupatikana kwa muafaka kati ya Wajumbe wanaounda Umoja wa
Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA na Chama cha Mapinduzi CCM,baada ya kupanga
mpango wa kuwazuia Wajumbe wa UKAWA,kutoonana na Rais Jakaya Kikwete ili kupata
Suluhu,Mtandao huu umedokezwa.
Mpango huo wa Kinana unakuja baada ya kikao
cha siri kati Msajili wa Vyama vya Kisiasa nchini,Francis Mtungi na wajumbe wa
UKAWA pamoja na wajumbe wa chama cha Mapinduzi kikao hicho kuvunjika na
kutopatikana kwa mwafaka,
Chama CCM,ambacho ni wapangaji katika
ikulu ya Tanzania,kimeamua kupanga mpango huo wa UKAWA kutokutana na Rais
Kikwete huku wakigopa kasi waliyokuwa nao,ambayo inaweza kubadilisha mwelekea
wa CCM,
Chanzo hicho kinasema Hofu ya Kinana
pamoja na chama chake inatokana na Wajumbe wanounda umoja huo wa UKAWA,kuwa na
nguvu na kuweza kushawishi Rais Kikwete na kuweza kuyakubali Mapendekezo hayo
na kuanza kuyatekeleza,
Mapendekezo hayo ambayo chama cha
Mapinduzi CCM,wanayahofia ni Pendekezo la UKAWA kutaka Rasimu iliyowasilishwa
Bungeni ambayo inaunga mkono Muundo wa Serikali tatu ijadiliwe na kutupia Mbali Rasimu ya kipropanga ya chama
cha Mapinduzi CCM,inayopigia chapuo muundo wa Serikali mbili.
Kitu ambacho
kinaweza kumfanya Rais Jakaya Kikwete kukubali pendekezo hilo na kupelekea
wajumbe wanaunda ukawa kurudi Bungeni,na kukiacha chama chake kikiangaika.
Wingu,zito bado likiwa limetanda
ndani ya chama cha Mapinduzi CCM,kuhusu ni hatua zipi zitumike hili kuokoa
mchakato huo wa Katiba mpya ,ambao unaonekana kutoweza kupatikana kutokana,hatua
iliyoko sasa ambayo baada kila upande kutopatiwa ufumbuzi huku kukiwa na
jitihada za kuokoa mchakato huo zinazofanywa na msajili wa vyama vya Kisiasa
nchini kugongwa mwamba.
Hoja ya UKAWA kutaka kujadiliana na
marais wawili ililenga kumpa fursa Rais Kikwete kurejesha nyuma msimamo wake
kuhusu rasimu ya pili ya katiba, maana siku alipozindua Bunge la Katiba,
aliweka msimamo ambao ndio umekuwa ukifuatwa na wajumbe wote wenye maslahi na
CCM.
Mara kadhaa, baadhi ya watu mashuhuri
na taasisi zimesema kwamba kama Rais Kikwete asingeleta msimamo wa chama chake
bungeni, ingejadiliwa rasimu ya tume, na UKAWA wasingetoka.
Miongoni mwa watu maarufu
waliokiri kwamba rais alikosea ni pamoja na Msajili ya Vyama vya Siasa mstaafu,
John Tendwa, ambaye alikiri kwamba rais aliteleza.
Jumuiya ya Wakristo Tanzania (CCT)
ilitoa waraka wake kusisitiza hoja hiyo, kwamba kauli ya rais ndiyo ilivuruga
mchakato, na kwamba ili Bunge liendelee kwa amani inabidi wajumbe wote
wajielekeze kwenye rasimu ya pili ya katiba iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Mara kadhaa, viongozi wa UKAWA
wametamka wazi kwamba iwapo mjadala wa Bunge hilo hautajikita katika rasimu
hiyo, hawatarejea bungeni.
Serikali imekuwa inafanya jitihada
za chini chini, na za wazi kuhakikisha wajumbe wa UKAWA wanarudi bungeni,
lakini wao wanadai kwamba hawawezi kurudi kujadili rasimu ya CCM badala ya
rasimu ya wananchi iliyowasilishwa na Jaji Warioba.
No comments
Post a Comment