NI HUZUNI----HALI YA MSANII BAHATI BUKUKU YAZIDI KUWA MBAYA SANA,SASA HAWEZI KUKAA WALA KUTEMBEA SOMA HAPA KUJUA KWANINI
Pichani ni Msanii wa Nyimbo za Injiri Bahati Bukuku akiwa amelezwa,
Na Karoli
Vinsent
HALI ya
Msanii Hodari wa Nyimbo za Injiri Nchini Tanzania Bahati Bukuku inazidi kuwa
mbaya,sasa kinachoitajika ni Maombi na sara kutoka kwa Watanzania ndio itakayoweza
kumwokoa Msanii huyo wa Injiri,Mtadano umeambiwa.
Bahati Bukuku,ambaye alipata ajari
mbaya ya Gari iliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita kwenye eneo la Ranchi ya Narco wilayani
Kongwa Mkoani Dodoma m,ajira ya saa tisa
usiku wakati alipokuwa anakwenda Mkoani Shinyanga,Kahama kwenye mkutano wa Injiri
ambapo ajari ndiyo iliomleta matatizo makubwa.
Akizungumza na Mwandishi wa Mtandao
kwa Njia ya Simu Rafiki wa karibu wa
bahati Bukuku,ambaye akutaka kutaja Jina kwenye Mtandao huu kwa kusema yeye sio
msemaji wa Familiya Bukuku alisema kwa sasa hali ya Bahati bukuku inazidi kuwa
mbaya sana na sasa kinachoitajika ni
sara na Maombi tu.
“Da leo nimeoka kumwangalia Hospitari
yaani da hali ya Rafiki yangu Bahati Bukuku ni mbaya sana na kinachoitajika
sahivi ni maombi tu,maana ukimwangalia mpaka unapatwa na huruma sana tena
unapata maswali ya kujiuliza huyo ndio msanii mwenye afya tele juzi tu?”alihoji
mpashaji huyoHabari.

Pichani ni gari alikuwa akilitumia Msanii Bahati Bukuku
Mwandishi wa Mtanda huu
alipomtaka Rafiki huyo ataje kitu gani kinachopelea hali yake bahati bukuku
kuwa mbaya,
“Bahati ameumia sana kwenye kiuno na
ukimwangalia utajua Kiuno kimevunjika na sehemu zengine ikiwemo Shingo hawezi
kukaa wala kutembea yeye amekuwa mtu wa Kulala tu,na kinachoitajika sahivi ni
sara tu sio kitu kengine maana uwezekano wa kupona ni mdogo sana”alisema mtoa
huyo taarifa.
Msanii Bahati Bukuku,ambaye anatamba nyimbo kadhaa ikiwemo Dunia haina
Huruma,Maamuzi pamoja na Majaribu ambapo katika Ajari hiyo Dereva wa Gari aliyokuwa anasafilia haina ya
Toyota Nadia lenye namba za usajili T 7945 Edsoni Mwakabungu “EDY” Miaka 31
ambaye ameumia Vibaya sana na Vidole na pia hawezi kutembea kabisa
Watu wengine waliokuwemo kwenye
Ajari hiyo ni Wacheza shoo wa Bahati
Bukuku Franki Muha (20) na mwenzake kwa Jina halikupatikana mala moja.
Naye Bahati Bukuku alinikuliwa na
Mtandao mmoja wa Habari huku akisema kwa shida sana alisema kwa sasa hali yake
ni mbaya sana na kuwataka watanzania kumwombea ili apone na aje kuendelea na
kazi yake ya kuendeza Injiri.
Msanii huyo ambaye ni Mwenyeji
Mkoani Mbeya kwa sasa bado amelazwa Hospitari ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar
es Salaam .
No comments
Post a Comment