TCU YADHAMILIA KUONDOA SINTOFAHAMU ILIYOJIKITA KATIKA MIOYO YA WADAU WA ELIMU tANZANIA, NI KUHUSU MATOKEO YA HIVI KARIBUNI YANAYOUMIZA VICHWA VYA MAMILIONI YA WATANZANIA
Tume ya vyuo vikuu hapa nchini TCU inatarajiwa kukutana na wadau wa elimu wa hapa nchini na wale wa kimataifa ili kujadili mustakabali wa elimu ya Tanzania ambayo kwa sasa Watanzania walio wengi wanaona kama inakua kwa kasi ya kimbunga huku wahitimu wake wakiwa hawajiwezi katika suala zima la kukabiliana na maisha huko Mtaani
Akizungumza na mtandao huu mapema hii leo kaimu katibu mtendaji wa Tume ya TCU Prof. Magishi Nkwabi amebainisha wazi kuwa lengo la mkutano huo ni kutaka kujua na kujipima ni namna gani tufanikiwa katika kukamilisha malengo ya millenium ambapo lengo lake ni kuona kila mtanzania anapata walau elimu ya kutosha na hivyo kulifanya taifa kuwa la uchumi wa kati ifikapo 2025
Katika mkutano huo utakaowashirikisha waajiri, inadaiwa waajiri watapata fulsa ya kusema ni nini hasa soko lao linahitji kuhusu rasilimali watu ili vyuo vyetu hapa nchini viweze kutengeneza mitaala itakayokwenda sambamba na mahitaji ya waajiri huko sokoni,
Tumeona ni vyema kwanza tukajua hasa waajiri wanataka watu wenye ujuzi upi na mahitaji hao tuweze kuyatengenezea utaratibu utakaowasaidia wahitimu wetu kupata fulsa ya kuajiriwa huko sokoni,
Akizungumzia kuhusu mafanikio ambayo kwa sasa tayari TCU imeyapata, Prof. Nkwabi amekili kuwa kwa sasa elimu ya Tanzania inafanya vizuri sana ukilinganisha na miaka mingine kwani kuna jitihada kubwa zimefanyika kuhakikisha wanafunzi wengi wanapata fulsa za kujiunga na vyuo vikuu kupitia njia ya Mtandao ambapo hapo awali ilikuwa ngumu kwa wanafunzi kupata fulsa ya kuomba na kupatiwa chuo kwa wakati na hivyo wanafunzi wachache walikuwa wanapata nafsi ya kujiunga na kozi mbalimbali katika vyuo vyetu.
| Waandishi wa habari wakiwa makini kuchukua dodoso toka kwa maprofesa walikuwa wakizungumzai mkutano huo |
No comments
Post a Comment