KWA HERI MABILIONI YA USWISI,SASA WATANZANIA WATEGEMEE MIUJIZA ILI PESA HIZO ZIRUDI,SOMA HAPA KUJUA KWA NINI
Pichani ni Mbunge Kigoma Kaskazini CHADEMA Zitto Kabwe picha na Maktaba
Na Karoli
Vinsent
UWEZEKANO wa
Mabiloni ya Fedha yaliyofichwa na Vigogo kwenye Mabenki mbalimbali nchini
Uswizi,sasa inazidi kuwa ni ndoto kwa fedha hizo kurudi kutokana na kutokuwa na nia ya Dhati ya Serikali ya Rais
Jakaya Kikwete kufanikisha Fedha hizo kurudi nchini,Mtandao huu umebaini.
Sakata la Mabilioni hayo ya Uswisi
yaliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe,ambaye naye kwa sasa
ameoneka kama kufungwa mdomo kwenye sakata hilo la kupambana ili fedha hizo
ambazo ni chafu ili zirudi nchini.
Kwa mujibu wa Vyanzo mbalimbali
zinasema zaidi ya bilioni 200,zimefichwa na watanzania kwenye Mabenki
mbalimbali nchini uswisi,fedha hizo ambazo nyingi zimeonekana kufichwa na
viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge,mawaziri wa awamu ya tatu nay a Nne,viongozi
wa juu wazamani wa Jeshi, pamoja na wasaka urais ndani CCM
,
Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi
wa Mtandao huu,umebaini hakuna nia ya Dhati iliyofanya na serikali ya Rais
kikwete kutokana kupuuza ushauri unaotelewa na watu mbalimbali ambao waliweka
mipango ya kuhakisha fedha hizo zinarudi ili zije kuwanufaisha watanzania ambao
wanaishi kwenye lindi la umasikini wa kutupwa
Upuuzi wa kwanza uliofanywa na Serikali
ya Rais Kikwete katika sakata hili ni pale ilipokataa ushauri uliotolewa na
Jaji mmoja kutoka Ufaransa ,Renaud Van Ruymbele kuhusu hatua ambazo zinatakiwa
kufaata ili kuwabaini watu walioficha pesa hizo kwenye Akaunti mbalimbali za Mapenki huko Uswisi.
Jaji huyo ambaye anasifika katika
Masuala hayo kutokana na Jinsi alivyoweza kuwabaini Akaunt za wafaransi nchini Uswisi
ambao walikwepa kulipa kodi.
Jaji huyo Aliidokeza Serikali ya
Tanzania kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Mahesabu ya Serikali (PAC) Zitto Kabwe
kwamba taarifa zote kuhusu Watanzania,Alishauri kwanza Serikali ya Tanzania
ipeleke Barua ya Maombi kwenye serikali ya Ufaransa ikiwemo wizara ya Sheriaya
Ufaransa.
Na endapo Tanzania ikifanya hivyo
Kikosi cha kazi kutoka wizara hiyo chini wa jaji huyo wataanza kufuatilia pesa
hizo zilizopo nchini uswisi
Lakini licha ya Serikali ya
Tanzania kupewa ushauri huo,lakini kile kinachonekana ni kupuuza ushauri
huo,ambao utapeleka pesa hizo kuwa ndoto kulejea kurudi nchini ni kutokana na
kitendo alichokifanya wiki iliyopita.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali nchini Fredilick Werema aliponukuliwa na Shirika la Habari la
Uingereza(Reuters) akisema kwamba
serikali inafuatilia “Suala la urejeshwaji wa Fedha hizo kupitia taasisi moja
Binafsi inayoitwa ISCAR iliyopo Basel uswisi ambayo inafanya kazi hiyo ya
kurudisha fedha hizo kwa Garama Kamisheni kubwa sana kwa serikali.
Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa
mtandano huu umezidi kugundua ni ndoto fedha kuzidi kurudi kutokana Taasisi
hiyo ISCAR iliwai kulalamikiwa na serikali ya Nigeria kwa kufanya kazi kusuasua
,ufuatiliwaji wa Mabilioni yalifichwa na kiongozi Dikteta Sani Abacha.
Duru za kisiasa zinasema ni ukweli
usiopingika kwamba Serikali ya CCM,inazidi kufanya maigizo kwa Watanzania
kuhusu suala hili kwani imekosa nia ya Dhati ya kufanikisha pesa hizi nyingi
zirudi nchini kutokana na watu wengi walioficha Fedha hizo huku Uswisi kuhusika
katika maamuzi mbalimbali ya sheria hapa nchini.
No comments
Post a Comment