Kamishina
wa polisi kanda maalum ya Daresalaam Suleimani Kova akitoa ufafanuzi jambo kwenye mkutano na waandishi wa Habari Jijin Dar es Salaam,
Na Karoli
Vinsent
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam
limefichua Siri ya kuongezeka Vitendo vya
ujambazi katika maBenki mbalimbali hapa nchini na kusema vitendo hivyo
vinasababishwa na Wamiliki wa Mabenki hayo kulipuuza Jeshi la polisi,
Kauli hiyo ya Jeshi la polisi Kanda ya Dar
es Salaam imekuja SIKU moja kupita baada
ya watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi kuvamia katika Benki ya Stanbic tawi la
Kariakoo liloko mtaa wa Swahili na kukomba mamilioni ya pesa aliyokuwa nayo
Mteja,
Kauli hiyo imetolewa Mda huu na Kamishna wa
Polisi kanda Maalum Dar Es Salaam,Suleiman Kova wakati wa Mkutano na waandishi
wa Habari Jijini Dar Es Salaam,ambapo alisema watu wanaochangia Vitendo hivyo
vya Ujambazi kuzidi kuongezeka katika Mabenki mbalimbali hapa nchini ni
Wamiliki wa Mabenki kupuuza ushauri wa Jeshi la Polisi ,
Uliowataka waache kutumia walinzi wa
Makampuni Binafsi peke yake,watumia na Walinzi kutoka Jeshi la polisi.
“Nataka niwambie waandishi hivi
vitendo vya Uvamizi kwenye mabenki
viemtokana na wamiliki wamabenki hayo kupuuza ushauri wetu uliowataka
kwenyes shuhuri za Ulinzi kwenye mabenki watumike Polisi tu,lakini wao wakapuuza,ukitaka
kuamini Nenda kwenye Mabenki yanayolindwa na Polisi kama utaona kama
kunauvamini wowote uonotokea,kwasababu majambazi hao wanashindwa kuvamia
kutokana na umakini wa Jeshi la Polisi”alisema Kova
Kamishna Kova,alisema kwa sasa Jeshi
la polisi limejipanga kuongea na Benki kuu(BOT) ambaye ni kiongozi wa Benki
zote hapa nchini na kutafuta ufumbuzi wa hili tatizo la Mabenki Mengine kupuuza
ushauri huo wa Jeshi la polisi.
Vilevile jeshi hilo la Polisi Kanda maalum
ya Dar es Salaam, Limeeanza msako kali wa kuwatafuta Majambazi watano waliovamia
Jana kwenye Beki ya Stabinc Tawi la Kariakoo lilioko mtaa wa Shwahili majira ya
mchana.
Kwa Mujibu wa Kamishna Kova alisema
watu wa tatu kati yao waliingia ndani ya Benki hiyo wakiwa na Mifuko Mikubwa
wakijifanya ni wateja wanapeleka Fedha nyingi katika Benki hiyo,watu hao
walipoingia ndani walianza kuwalazimisha kuvuka wigo wa wateja wa kwaida na
kutaka kuingia kwa nguvu kupora Fedha.
Ambapo Benki hiyo ya Stabinc ina
mitambo ya Aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vingora vya Tahadhari,ikasaidia
kwa majambazi hao kushindwa kuingia ndani kuiba pesa za Benki hiyo kutokana na Vingora
hivyo kupiga kelele na kuanza kuwapa uwoga majambazi hao ,ambapo walifanikiwa
kuiba pesa za mteja mmoja ambae alikuwa anataka kuweka pesa kwenye benki hiyo,
Kova alisema Majambazi hao
walipotoka nje ya Benki hiyo walipiga Risasi Juu ili kuwapa Hofu wananchi
walikuwa Nje ya Benki hiyo,ambapo kwa Mujibu wa Kamishna Kova anasema bado
wanaendelea kuwafuatilia majambazi hao.
Katika Hatua nyingine Jeshi hilo
la polisi Limejipanga ipasavyo kwenye sikuku ya IDD El Haji 2014,ambapo jehi
hilo limesema limepanga kushikirikiana na Vyombo mbalimbali vya ulinzi na
Usalama ikiwa ni pamoja na Kikosi cha
Zima Moto na Uokoaji,Kampuni Binafsi za ulinzi lengo ni kuhakikisha wananchi
wanafurahia kwa utulivu na amani kwenye sikuku hii.
|
No comments
Post a Comment