Zinazobamba

HABARI ILIYOTIKISA JII,Madini ya "URANI"ni kabuli linalochibwa kuwazikia watanzani, wananchi watoa kauli nzito

Wakili Flavina Charles akifafanua jambo mbele ya wadau wa GDSS katika mkutano maalum wa kuzungumzia madini ya Uranium, Katika mkutano huo Falviana ametoa ushuhuda wake juu ya athari ya madini ya Uranium na kusema madini hayo yakichibwa ni sawa na kuwachimbia kaburi watanzania huku faida zinazotajwa za umeme na ajira zikiwa hazina mtumiaji.

Kaburi!kaburi!kaburi, hayo si maneno yangu ambayo nayaandika katika habari hii, bali ni maneno mazito toka kwa wanaharakati ngazi ya wananchi ambao wamekusanyika katika viwanja vya TGNP kujadili hatima na madhara ya uchimbaji wa madini aina ya Urenium ambayo serikali tayari imeshakubali utoaji wa lezeni yae,
Kaitika kikao chao hicho kilichotumia masaa zaidi ya mawili wananchi hao wamekuja na kauli mbiu moja ya kuitaka serikali kuachana na mpango wa kuchimba madini ya Uranium Wakisema kuwa uchimbaji wa madii hayo ni sawa na kumchimbia kaburi mlala hoi ambaye madhara yakitokea hawezi kukimbia kwenda kokote huku wanasiasa wakiweza kufanya hivyo kwai wanakinga ya kidiplomasia,

Wananchi hao wamesema hoja ya kwamba uchimbaji wa madini hayo ni muhimu kwa kuweza kulifanya taifa kupata umeme wa uhakika na kutengeneza ajira kwa vijana wetu si kweli kwani tuna vyanzo vingi vya kutengeneza ajira pamoja na huyo umeme unaodaiwa na hiyo serikali,
Wameongeza kusema kuwa, habari ya kutulazimisha mikataba ya uchimbaji wa Uranium haikubaliki hata kidogo kwani tunajua wazi kuwa uchimbaji wake uaathiri afya zetu na vizazi vyetu vijavo,
 Hivi huo umeme na ajira ni kwa ajiri ya nani hasa?? kama wananchi wote wataathirika na wengine kuugua kansa za vizazi na wengine kuwa vipofu hivi kunahaja gani ya kuwa umeme ambao hakuna mtumiaji wake Aliongeza mmoja wa wanaharakati hao wa kazi ya jamii maalufu kama GDSS 

Akiwasilisha mada kwa wananchi kuhusu madhara ya madini ya Uranium, Mwanasheria na Makam wa rais wa Chama cha wanasheria wa Tanganyika, Wakili Flaviana Charles amekiri waziwazi kuwa madini ya Uranim yana madhara makubwa ukilinganisha na faida zinazoelezwa na serikali kila Leo.
Madini haya ya Uranium ni hatari sana, kwanza uchimbaji wake sio rafiki kwa mazingira kwani mahandaki ya mashimo tutayashuhudia kuyaona huku vifusi vingi tukishindwa wapi kwa kuvipeleka, Mbali na hilo Mionzi ya madini haya ni hatari kupita maelezo kwani mtu ikimkuta ujue lazima afe na kama hajafa basi maini yake yatatoboka na kuharibu kabisa uzazi wake na hivyo kushindwa kuzaa wala kuzalisha hatua ambayo ni mbaya kabisa,
Ameendelea  kubainisha kuwa, kama tusipokuwa makii na kutunza madini haya yasichimbwe, basi kuna uwezekano wa tanzania chima kukawa na makaburi ya watu walioathirika na madini haya kwani minzi yake pia unaweza kuipata kama utakunywa maji ambayo yamepitiwa na mionzi hiyo,
Hebu niambie wewe Mtanzania utaponea wapi kwan maji yote ambayo tunayatumia yanatiririshwa toka mito mbalimbali, sasa mito hiyo pia inakutana katika maungio yao hivi huoni kwamba utahatarisha taifa zima, ni bora tusichimbe kabisa na tukaangalia vyanzo vingine vya kutengeneza umeme,Aliongeza wakili Flaviana.

Hakuna maoni