MSIKITI WA AINA YAKE WAZINDULIWA DAR, NI BONGE LA MSKITI, JIONEE MWENYEWE HAPA
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akikata utepe kuzindua
rasmi Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliojengwa na mfanyabiashara maarufu
nchini, Said Salim Bakhresa katika eneo la Uwanja wa Chamazi, Mbagala
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti huyo wa Makampuni ya SSB,
Said Salim Bakhresa, ambapo pia uzinduzi huo uliofanyika leo Julai 4,
2014, ulihudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Kiserikali akiwemo na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
na wengineo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na wenyeji wake wakati alipowasili Msikiti wa ‘Masjidil
Huda’ uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhudhuria
uzinduzi wa msikiti huo uliofanyika leo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (wa pili
kushoto) Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ( wa pili kuli)
Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa (katikati) na Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto) wakijumuika
na waumini wa dini ya Kiislam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkititi wa
‘Masjidil Huda’ na Swala ya Ijumaa uliofanyika leo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni