MKUU WA CHUO MUHUJUM UCHUMI AFIKISHWA KORTINI,
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Profesa Johannes Monyo na wenzake sabawamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakituhumiwa kwa makosamanne tofauti yakiwemo ya uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali kiasi cha Sh 6,258,448.60.
Profesa Monyo na wenzake walisomewa mashtaka manne tofauti janamahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka Adam Kilongozi aliyekuwa pamoja na Hamidu Singano.
Katika shikata la kwanza, Profesa Monyo na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi chuoni hapo, Jerome Augustino inadaiwa kuwa Septemba 30, 2011 wakiwa waajiriwa kwa nafasi zao walizitumia vibaya kwa kubadilisha matumizi ya vifaa vya umemejua (solar) kwa manufaa yao binafsi.
Aidha, katika shitaka la pili wanaohusishwa ni Jerome Agustine, Chacha Wambura, Mpoki Mwasaga, Papias Njaala, Mathew Melita, Mary Thomas, Elisaria Kisanga na Gerald Malisa ambao inadaiwa kuwa, kwa pamoja wakiwa wajumbe wa bodi ya manunuzi walitumia nyadhifa zao vibaya na
kuidhinisha manunuzi ya sola hiyo yenye thamani ya Sh 6,258,448.60 kwa kutumia utaratibu wa kuipa zabuni kampuni ya Helvetic Solar Contractrors .
Katika shitaka la tatu, watuhumiwa Augustino ,Faraji Mnyepe na Honory Mkelemi kwa pamoja inadaiwa kuwa kati ya Novemba 1 na 30 mwaka 2011 katika utekelezaji wa majukumu yao, kila mmoja waliwezesha mchakato w malipo kwa kampuni ya sola ya Helvetic Solar Contractors kwa kutoa
malipo ya Sh 6, 258,448.60

Na shitaka la nne, Profesa Monyo na Augustine wanadaiwa kuwa mnamo na Novemba 30 /2011 wakiwa waajiriwa chuoni hapo kwa nyadhifa tofauti,
walikisababishia hasara chuo hicho cha uhasibu kiasi cha Sh 6,258,448.60.
Baada ya kusomewa mashataka hayo na mwendesha mashitaka Kilongozi, washitakiwa wote walikana mashitaka yao na hakimu wa Mahakama hiyo,
Mustapher Siyan alitoa masharti ya dhamana ambayo ni kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wafanyakazi wa serikali na kusaini bondi ya sh
milioni 1.
Hata hivyo washtakiwa hao wote walitimiza masharti ya dhamana, huk hakimu akitoa amri ya kukamatwa kwa washitakiwa wengine watatu ambao ni Mwasaga, Melita na Malisa ambao hawakufika mahakamani hapo.
Aliagiza popote walipo wakamatwe ili kufikia Agosti Mosi wafikishwe mahakamani hapo kusomewa mashitaka yao.
Awali kabla ya kusoma kwa kesi hiyo ndani ya chumba cha mahakama baadhi ya watumishi kutoka chuoni hapo walitaka kuwadhibiti waandishi wa habari ambao ni wapiga picha za video wasifanye kazi zao, lakini wanahabari walishinda kutokana na kuwa na kibali cha kupiga picha mahakamani hapo.
SOURCE MPEKUZI
Hakuna maoni
Chapisha Maoni