Zinazobamba

BAADA YA MAJAMBAZI KULITIKISA JIJI LA DAR LEO-HII NDIO SABABU YA MATUKIO HAYA KUZIDI KUSHAMILI KATIKA JIJI HILI SOMA HAPA UJUE SABABU



Sehemu ya uhalibifu uliofanywa na Majambazi hao katika gari la Magereza leo Jijini Dar es Salaam

Na Karoli Vinsent
 MATOKEO ya Dharau inayofanywa na Vyombo vya usalama ndani ya nchi,kuhusu taarifa zinazoripotiwa kwenye vyombo vya Habari  ikiwemo magazeti na Mitandao, juu Jambazi mwenye uraia wa Nigeria ambaye amekuwa akifanya Uharifu huku, Jambazi huyo akijinadi kwamba hakuna wakuchukulia hatua hapa nchini,matokeo yake  yaanza kuonekana.
               Matokeo haya yameonekana leo wakati wa Tukio la Ujambazi lilotokea Maeneo ya Mikocheni Jijini Dar Es Salaam karibu na Hoteli  ya Rigency,ambapo Kundi la watu wanaodhaniwa ni Majambazi kuvamia Gari lilokuwa na Fedha ambalo lilikuwa karibu na hoteli hiyo, ambapo gari hilo lilikuwa kwenye Foreni ndipo wakatokea Majambazi ambao waliokuwa kwenye Pikipiki na kulifuata gali hilo ambalo lilikuwa na Mtu mwenye Fedha na kumwamulu ataoe fedha hizo.
           Ambapo wakati majambazi hao wakimwamulu Jambazi huyo atoe fedha,na mtu huyo kutoa Fedha ndipo pembeni mwa Majambazi hao kulikuwepo na Gari la Jeshi la magereza ambalo lilikuwa limewapakia wafungwa,ambapo Askari wa magereza walipoona tukio hilo ndio wakatoa Risasi na kuanza kuwarushia Majambazi hao ambapo Majambazi hao wakajibu mashambulizi na kupelekea kuvuja vioo vya Gari hilo,na kufanikiwa kukimbia Majambazi hao na Fedha.
             

Sehemu ya uhalibifu uliofanywa na Majambazi hao katika gari la Magereza leo Jijini Dar es Salaam.


       Kuendelea kwa Matukio haya ya Ujambazi kumekuja Siku chache baada ya Mtandao huu,pamoja na Gazeti moja linalotoka mala moja kwa Wiki kufichua mtandao wa majambazi,ambao unaongozwa, kiongozi anajulikana kwa jina Kingsley O.Ugiagble ambae amekuwa akifanya ujambazi ndani ya nchi pamoja na kumiliki  mtambo wa kutengeneza Fedha za Kimarekani “Dola” pamoja na za Ndani vilevile kufanya wizi kwenye Hudama za Benki ATM.
        Huku Vyombo vya Usalama vikidhalau Taarifa hiyo,Kingsley ambaye amekuwa akimiliki makundi kadhaa ya kijambazi hapa nchini huko wahusika wakimfumbia macho .
Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa Mtandao huu umebaini Jambazi huyo mwenye Asiri ya Nigeria ambaye anakaa Maeneo mbezi jijini Dar es Salaam,kwenye nyumba ambayo yenye Thamani ya milioni 250,jambazi huyo amekuwa akihusika na mtandao wa kutenganeza fedha feki za kimarekani yaani Dora.
        Chanzo hicho cha Habari kilizidi kusema Kingsley amekuwa amekuwa anahusika kuleta Silaha ambazo zimekuwa zikitumika katika Vitendo vya Ujambazi hapa nchini,huku mamlaka zikishindwa kumchukulia hatua.
Kingslaye ambae amekuwa akijinadi kwamba hakuna wa kumchukulia hatua kutokana kujuana na Wataendaji wakubwa ndani ya Idara za usalama wa nchi,hatahivyo chanzo hicho cha Habari kilimtaja jamabazi huyo kuhusika kumiliki mitambo miwili ya Kutengeneza Fedha Bandia ambayo hutumika kutengeneza noti ya sh 10000.
        Ambapo mtambo mwengine unatengeneza Dola za Kimarekani ambazo sio rahisi kuzitambua.Taarifahiyo inasema fedha hizo zipo kwenye mzunguko wa Fedha kwa maana zikipitishwa kwenye utambuzi maramoja ni vigumu kuzitambua mpaka utakaporudia marambili ndipo  mashine hiyo utambuzi itagoma.
      Uchunguzi wa  Mwandishi wa Mtandao huu amebani Mtambo huo wa kutengeneza Fedha hizo bandia unahifadhiwa katika nyumba moja maeneo ya Kunduchi jijini Dar es Salaam na kuendelea na mpango wake wa Kudurufu Fedha hizo huku Idara za Usalama zikimwogopa Jambazi huyo.
Kingsley,ambaye ameingia nchini kutoka nchini Nigeria pasipokuwa na Pasipoti wala bila hata fedha yeyote ambapo amekuwa akipata fedha nyingi kutokana na hujuma hiyo anayofanya ndani ya nchi kutokana vitendo hivyo vya kijambazi.
         Kwa mujibu wa Vyanzo vya kuamika zinasema Jambazi Kingsley kabla ya kuja nchini aliwai kufanya vitendo hivyo vya Ujambazi katika Nchi za Ghana,Kenya pamoja na Nigeria,ambapo hivi sasa amehamina nchini na kuendelea na vitendo hivyo.

Hakuna maoni