WANAHARAKATI NGAZI YA JAMII WAISASAMBUA BAJETI YA TILIONI 19.9,WASEMA SI RAFIKI KWA MTANZANIA
Mwezeshaji wa vikundi vya GDSS Bw. Badi Deus Akifafanua jambo ya wana GDSS |
Wanaharakati ngazi ya jamii wameitizama Bajeti ya Tilioni
19.9 kwa undani na kisha kutingisha kichwa na kutoa neno moja tu kuwa bajeti hiyo si rafiki kwa Mtanzania, Kisa ni bajeti hiyo kuonyesha wazi upendeleo wake kwa wawekezaji wa nje huku ikimsahau
mwananchi wa kawaida katika kumjengea uwezo ili ajikwamue na lindi la umasikini
unaomkabili kila kukicha,
Wanaharakati hao wameyabaini hayo baada ya kuifuatilia bajeti hiyo kwa muda mrefu, toka inawasilisha na hatimaye jana jioni walikutana na kuitangaza bajeti hiyo kuwa siyo bajeti rafiki kwa mwananchi wa kawaida,
Wanaharakati wa GDSS wakifuatilia kwa makini mrejesho wa vikundi mbalimbali vilivyochambua bajeti ya mwaka huu katika viwanja vya TGNP huko mabibo jijini Daressalaam |
Moja ya hojazilizowakwaza wana GDSS ni kuruhusu mwekezaji kupata unafuu wa maisha huku mtanzania akiendela kuumia na kodi kubwa wakati wao wawekezaji wakisamehewa kodi
Hata hivyo wamepongeza hatua ya serikali kukubali kuinusuru sekta ya elimu baada ya kutenga jumla ya MILIONI 500 kwa kila halmashauri, hatua iliyotafsiriwa kuwa ni nia ya dhati kuikomboa elimu iliyoteteleka kwa muda mrefu,
Nachangaia, mwanaharakati Neema Nsoro akitoa dukuduku lake kwa Wana GDSS hapo mabibo,Katika mkutano huo wa Wana gdss Uliwakutanisha jumla ya wanaharakati 100 toka mikoa mitano hapa nchini. |
Katika hatua nyingine, wana GDSS wamepongeza hatua ya serikali ya kumjali mzee wa Tanzania baada ya kukubali kumlipa mzee mstaafu wa Kitanzania jumla ya shilingi 50000 bila kujali kuwa alikuwa serikalini ama sekta ya umma
Hakuna maoni
Chapisha Maoni