ULAFI, NJAA UNAVYOMMALIZA MWANAJESHI TOKA JWTZ, AVUA MAGWANDA NA KUKIMBILIA LAKI TATU ZA SONIT
"Damian Sanya" Mgombea urais mwanajeshi aliyetundika makombati yake kwa muda. |
Unaweza kuuita kama ni Ulafi, ama njaa zisizo za lazima ambazo zimemukuma mwanajeshi shupavu ambaye ameweza kuaminiwa na nchi kupelekwa sudani kulinda amani, lakini bado hajalizika sasa ameaamua kuvua gwanda na kuingia msituni kuitafuta laki tatu ya kila mwezi toka serikali ya wanafunzi ya sonit,
Watafiti wa mambo wanasema hatua ya mwanajeshi kugombea nafasi ya urais Chuo cha taifa cha usafirishaji haikulenga kumsaidia mojakwa moja mwanasonit na badala yake Mwanajeshi huyo amelenga kujilimbikizia mali kwa njaa zake ambazo hazina kikomo,
Mpaka hii leo tayari mwanajeshi huyo gumzo katika chuo cha taifa, ameshakuwa na watu ambao inasadikiwa amewanunua ili waweze kuhakikisha dhamira yake hiyo ya kukiteka chuo kwa staili ya kijeshi inafanikiwa na tayari watu taratibu wanaonekana kuanza kumtilia shaka juu ya dhamira yake ya kutaka kuwa mtawala wa wanafunzi na hizi hapa ndio sababu zinazowafanya wanasonit wawawze mara mbili juu ya Mgombea huyu ambae hafahamiki hata tabia yake kwa watu kuanza kutaka kutawala umma wa Sonit
- Kwanini mwanajeshi atake kutawala NIT, na ikizingatiwa kuwa yeye ni mwajiriwa wa serikali ambaye muda wowote akitakiwa ni lazima aitikie wito na wala sio Ombi,
- Mpaka leo Tayrai mwanajeshi huyo alitupa kombati anafaidika na mikopo huku akilipwa mishahara mbalimbali na serikali, kwa nini anaamua kuzikodolea macho 300,000 Za wana sonit kama yeye kweli si mrafi
- Umeshawi jiuliza utawala wa kijeshi unakuwaje?????, hakika mtawala huyu alijivisha ngozi ya kondoo kwa sasa ikifika amekaa katika kiti cha madaraka hakuna atakae kuwa na uwezo wa kusema hapana kwake na ikiwa hiyo nadhani atatumia intelijensia ya hali ya juu kumuondoa chuoni na hata wanafunzi wengine wasijue kwa nini imekuwa hivyo,
- Mwanajeshi kutawala Nit nazani kuna haja ya kuvua miwani yetu ya mbao na kuangalia mbele jamaa anataka nini hasa, Ni mwaka wa kwanza tu tayari, anajifanya anataka kutawala watu, hivi ni wakati wa nit kutawaliwa kijeshi, Alihoji Bakari Twahiru , mmoja wa wanafunzi wa Logistikia katika chuo hicho.
Kuna maswali mbalimbali ambayo wadau wamekuwa wakijiuliza huku wakikosa majawabu yake, Wengine wanasema Mwanajeshi kwa ilivyozoeleka na wengi huwa wanafundishwa utii sasa iweje huyu mwanajeshi aweze kutetea haki za wanafunzi ambao muda mwingine haki hudaiwa kwa migomo,
Hapo ndipo mwanajeshi huyo aliyekimbia mizinga nchini Sudani, ambako alipelekwa kwenda kulinda amani alipoamua kuvunja ukimya na kusema wazi kuwa jeshi kwake si lolote kwa sasa kwani tayari analikizo isiyo na nguvu ya kijeshi hivyo anauwezo wa kuongoza migomo kama chuo Cha Dit kilivyofanya,
Mimi si mjuzi sana wa mambo lakini ninavyojua jeshi likikutaka uende ukafanye yao si dhani kama mwajiriwa utagoma eti kisa unalikizo isiyo na nguvu ya Kijeshi, Huu ni uwongo tena wa dhahili hakuna kitu kama hicho hapa Tanzania na hata dunia kwa ujumla eti mwanajeshi akamgomea bosi wake,si dhani kwamba utetezi wa Sanya unamashiko kwa wana Sonit.
Wadau wa Mwanajeshi wakiwa mbele kutoa sapoti ya nguvu kwa utawala wa kijeshi nit, |
Gidion Geoge akifafanua jambo, Makam wa rais wa Tungalaza |
Hakuna maoni
Chapisha Maoni