Uraghbishi Wa TGNP waonyesha mafanikio makubwa kwa walala hoi,
Kazi iliyofanywa na mtandao wa jinsia Tanzania TGNP umeanza
kuonyesha mafanikio yake baada ya utafiti wa kiragabishi katika kata za
Kiroka,wilaya ya Morogoro vijijini,Kata ya Mondo wilaya ya Kishapu, Kata ya
Tembela mkoani Mbeya, Kata ya Nyamaraga Mkoani Mara na Kata ya Mabibo Wilaya ya
Kinondoni kuonyesha wazi dalili za mafanikio katika matatizo yao mbalimbali,
Akizungumza na Mtandao huu, Mkurugenzi Mtendaji Wa Mtandao
wa jinsia Tanzania, Bi. Lilian Liundi amesema katika tafiti ambazo Mtandao huo
umeziendesha umegundua matatizo mbalimbali, ambapo wananchi katika maeneo hayo
wameanza kuamka baada ya kuchokozwa na wawezeshaji toka katika mtandao,
MARJORIE MBILINYI WA TGNP AKIFAFANUA BAADHI YA MAMBO. |
Kenny Ngumuo Muwezeshaji katika warsha hiyo akifafanua jambo, Ngumuo anasema hivi ni kwa nini mwanamke anapotaka kujifungua ni lazima abebe ndoo ya kubebea taka maji zake, |
Mdau akisikiliza kwa makini hoja za wanaharakati wa kijinsia, katika warshahiyo wadau mbalimbali walisifia hatua ya serikali kupiga marufuku vigodoro, na kusema hatua hiyo imekuja katka wakati muafaka. |
Liundi anasema moja ya matatizo makubwa ambayo sasa
yanaonekana kupatiwa ufumbuzi baada ya wananachi kuchokoza kudai haki zao, ni
pamoja matatizo yaliyo katika sekta ya afya ambayo kila kukicha wananchi
hususani ngazi ya jamii wamekuwa wakilalamikia,
Anasema, katika kata ya Kiroka wananchi wamekuwa wakiteseka
katika suala la Afya, baada ya watendaji wa huduma ya afya kuwa wakaidi kwa
wagonjwa, lakini baada ya zoezi hili la uragabishi wananchi wameweza kuamka na
kudai haki zao hatua iliyosaidia kwa watendaji hao wa Afya kuanza kusikiliza
vilio vya wanakiroka kwa kuwajibika na kuwasikiliza shida zao,
Utafiti huo , umenda mbele na kuonyesha mafaikio makubwa
ambapo hapo awali kabla ya wananchi kuchokozwa ilikuwa ni vigumu kwa jamii hiyo
kufanikiwa, Na kutolea mfano wa kata ya Mondo Ambapo wananchi wa kata hiyo kwa
mara ya kwanza waliweza kuthubutu
kuandamana na kudai maji safi na salama wakati wa ziara ya Waziri mwenye
zamana ya maji hapa nchini Mh. Jumanne magembe
Uragbishi umesaidia Mbunge wa Kishapu kwa mara ya kwanza
kufanya ziara ya kikazi katika kata ya Mondo ambayo hapo awali iliachwa solemba
na wanachi waliendelea kuteseka bila kutokea kwa mtetezi juu ya shida zao,
Aidha, Mtandao huo wa jinsia hapa Tanzania umefanikiwa
kubadili jina la mtaa mmoja katika kata ya mabibo ambalo lilikuwa likimzalilisha
mwanamke, kwa mtaa huo kuitwa jina “la maumbile ya sili ya Mwanamke”, na sasa
mtaa huo umepewa jina zuri la “Mji
mwema” ambao sasa wakazi wa mtaa huo wameombwa kutumia jina hilo na kuachana na
majina ya zamani.
Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) uliendesha tafiti za
uragbishi kuanzia machi 9-31 katika kata tano za Kiroka, Mondo,Tembela,
Nyamaraga na Kata ya Mabibo ambapo katika kata hizo, mafanikio mbalimbali
yalionekana baada ya wananchi kuchokozwa na kuchokozeka
Hakuna maoni
Chapisha Maoni