Zinazobamba

SERIKALI YA INDIA YAGEUKIA WAGONJWA WA FIGO BONGO, YAGAWA MASHINE ZA FIGO YENYE THAMANI YA 24 MILIONI

http://www.mnh.or.tz/images/sliders/mwaisela.jpg

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili imepokea msaada wa Mashine ya kusafishia damu yenye thamani ya sh. millioni 24 kwaajiri ya wagonjwa wa figo Nchini.
Mashine itatumika kutatua matatizo ya wagonjwa wanao hitaji huduma hiyo hususani katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).

Akizungumza Dar es Salaam jana Barozi wa India Nchini Debnath Shaw alisema Serikali hiyo inalengo la kuendeleza huduma ya afya nchini.

Alisema mbali na hilo pia Serikali hiyo itaendeleza ushirikiano katika mambo mbalimbali yanayohusu afya.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Agnes Mtamwa alisema ujio wa mashine hiyo inaweza ikawa chachu ya kuwasaidia wagonjwa wengi zaidi ukijumuisha na mashne zilizo kuwa awali.

http://www.mnh.or.tz/images/sliders/muhimbili.jpg "Msaada wa mashine hii imekuwa ni wakati muafaka kwani Serikali inaendelea kutekeleza mikakati wa kuboresha na kuimarisha huduma za afya na kitengo cha huduma za figo," alisema Mtamwa.
Alisema katika hospitali hiyo kuna mashine za aina hiyo 16 ambapo hutumia kuwahudumia takribani wagonjwa 30 hadi 35 wenye matatizo ya figo kwa siku.

Mbali na hilo Mtamwa alieleza kuwa wamekuwa na uhitaji mkubwa wa mashine hizo huku wakikabiliwa na changamoto kubwa ya ongezeko la wagonjwa hivyo mashine hiyo itaweza kupunguza kwa kiasi kidogo.

Hata hivyo Mtamwa aliitaka Serikali hiyo kusomesha watalaamu katika eneo hilo ili waweze kutoa huduma huduma kwa ubora zaidi.

Mwisho

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili imepokea msaada wa Mashine ya kusafishia damu yenye thamani ya sh. millioni 24 kwaajiri ya wagonjwa wa figo Nchini.

Mashine itatumika kutatua matatizo ya wagonjwa wanao hitaji huduma hiyo hususani katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).

Akizungumza Dar es Salaam jana Barozi wa India Nchini Debnath Shaw alisema Serikali hiyo inalengo la kuendeleza huduma ya afya nchini.

Alisema mbali na hilo pia Serikali hiyo itaendeleza ushirikiano katika mambo mbalimbali yanayohusu afya.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Agnes Mtamwa alisema ujio wa mashine hiyo inaweza ikawa chachu ya kuwasaidia wagonjwa wengi zaidi ukijumuisha na mashne zilizo kuwa awali.

"Msaada wa mashine hii imekuwa ni wakati muafaka kwani Serikali inaendelea kutekeleza mikakati wa kuboresha na kuimarisha huduma za afya na kitengo cha huduma za figo," alisema Mtamwa.

Hakuna maoni