MIZENGO PINDA SASA MAJI YA SHINGO, LHRC, TLS WAMKATIA RUFAA ,WASEMA NI LAZIMA ATENGUE KAULI
Miongoni mwa mawakili wanaosimamia kesi hiyo ya Mh. Pinda na Mwanasheria mkuu wa Serikali Wakili Peter Kibatala Naye akifafanua jambo kwa waandishi wa habari |
Na Seemani Magari,
Uamuzi uliofanywa na mahakama kuu ya Tanzania wa kutupilia mbali kesi ya
msingi iliyofunguliwa na Kituo cha haki za binadamu wakishirikiana na Chama cha
wanasheria wa Tanganyika (TLS) dhidi ya Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda na mwanasheria mkuu wa serikali sasa imechukua sura mpya baada ya wanasheria
hao kutangaza hadharani kutoridhishwa na uamuzi huo
na hivyo kudhamiria kukata rufaa ili haki iweze kupatikana,
Wakizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, Jopo la
wanasheria toka chama cha wanasheria wa Tanganyika wamesema hatua ya mwanasheria mkuu wa serikali
kuwasilisha pingamizi mahakamani akidai kuwa maombi ya kumshitaki waziri mkuu
hayakukidhi vigezo ni ishara tosha ya kuona jinsi gani haki za binadam
zinavyokandamizwa,
Wanasheria hao wakiongozwa na wakili kiongozi katika kesi
hiyo, Wakili Mpale Mpoki, wamesema mwanasheria wa serikali anadai wanasheria
hatuna uwezo wa kisheria kudai
mahakamani kama taasisi kumtaka waziri mkuu kufuta kauli yake sababu akiitaja
ni kuwa taasisi haiwezi kuathirika moja kwa moja na watu ambao wangekuwa na
uwezo kisheria ni mtu binafsi ambaye angeweza kuathirika moja kwa moja na kauli
ya waziri mkuu, hivyo Kituo cha sheria na Chama cha wanasheria hawana haki ya
kimsingi kumsemea mtu mmojammoja,
Wakili mpoki anasema, hiyo kwa tafsiri ya haraka ni sawa na
kusema, hata ukiona mwenzako anapigwa hapo na kuonewa huna mamlka ya kuweza
kumsaidia kwa kupeleka kesi hiyo mahakamani kutokana na ukweli kuwa wewe
hujaathirika moja kwa moja na kipigo cha huyo uliyemuona, kitu ambacho sasa
tunadhani ni lazima ifike wakati tuseme inatosha,
Tumeamua kukata rufaa dhidi ya hukumu ya mahakama kuu ya
Tanzania, sisi tunaona ni haki kuwatetea watanzania kwa umoja wetu sasa
inapokuja suala la kusema hatuna haki sababu sisi ni taasisi sasa hilo ni
tatizo na lazima ipatikane jawabu lake, Ukizingatia kauli ya muheshimiwa waziri
mkuu ni sawa na sheria katika nchi hii.
Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 1/08/2013 kituo cha sheria na
haki za binadam(LHRC) NA Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) walifungua kesi
dhidi ya Mh. Waziri mkuu Wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda na Mwanasheri a mkuu wa
serikali kupinga kauli ya waziri mkuu aliyoitoa bungeni mnamo tarehe 20/06/2013
alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo,
Katika siku hiyo Mh. Waziri alinukuliwa akisema, “””Ukifanya
fujo,umeambiwa usifanye hiki, ukaamua wewe kukaidi utapigwa tu. Eeh, Maana
hakuna namna nyingine. Eeh, maana lazima tukubaliane kuwa nchi hii tunaiendesha
kwa misingi ya kisheria. Sasa, kama wewe umekaidi hutaki, unaona kwamba ni
imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi watakupiga tuu na mimi nasema muwapige tuu
kwa sababu hakuna namna nyingine, Eeh, maana… maana tumechoka sasa””
Naye,Makam wa rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika
hapa nchini, Wakili Fraviana Chalres, ameonyesha kufurahishwa kwake kwa kitendo
cha Mahaka kuu hapanchini kuondoa kinga kwa wabunge na kusema kuwa hatua hiyo
ni mafanikio makubwa ya kujivunia katika vita ya kuwatetea wananchi hasa wale
walala hoi,
Fraviana amesema, Katika kesi ya msingi ambayo waliipeleka
mahakama kuu, moja ya mashitaka yao ni kwamba ibara ya 100 ya katiba ya
jamuhuri ya muungano wa Tanzania, 1977 au sheria nyingine yeyote isitumike kama
kinga dhidi ya wanaovunja katiba
Katika majibu ya msingi ya mahaka,ya mnamo tarehe 6june
2014,baada ya kupitia pande zote mbili, sasa ibara ya 100(2), inaweka mipaka na
ukomo wa kinga za bunge kitu ambacho kituo
cha sheria na haki za binadamu pamoja na chama cha wanasheria wa Tanganyika
wamsema kitasaidia sana katika kulinda haki za wanachi.
Ankali akiwa kazini |
“”sisi kama LHRC na TLS tumepokea uamuzi huo na tumeridhika
na tafsiri ya mahakama kuhusu ibara ya 100(2)kwamba kinga ya wabunge ina mipaka
na ukomo kisheria na inapaswa kuzingatia katiba na sheria zingine za nchi,
hivyo kinga hiyo inaweza kuhojiwa mahakamani, kitu ambacho ni muhimu sana
katika kujenga misingi ya haki za binadam, utawala sheria na utawala bora,””
Walisema.
Maoni 1
Ni kweli kinachotakiwa n hiyo kaui ifutwe hina tija na inaleta shaka iwapo kuna heshima ya utawala a sheria nchini
Chapisha Maoni