watumiaji wa smart fones washuriwa kutumia chaji za PUKU kwa usalama wa simu zao, T
CORE founder of Puku AKIONYESHA CHAJA MUHIMU KWA SIMU ZA SMART FONES. |
WATUMIAJI wa simu za
kisasa za Smart Phone wametakiwa kutumia chaji za Puku kuchajia simu zao ili
kujihakikishia usalama wake.
Akizungumza na waandishi wa habari
katika uzinduzi wa chaji hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUKU alisema
kuwa chaji hizo kwa sasa zinapatikana hapa nchini.
Alisema kuwa ni chaji ambazo zinahifadhi
umeme kwa muda mrefu ambao unakuja kutumiwa kuchajia simu hasa pale ambapo
panakuwa hakuna umeme.
Aliongeza kuwa bei yake kwa sasa ni
kuanzia 160,000 kutokana na ubora wake na pamoja na namna ambavyo inasaidia.
"Mimi ni mtanzania kutoka Tanga
na nilisoma hapa hapa ila nilielekea Marekani kusoma na ninaishi huko na
nimebuni hii chaji kwa lengo la kusaidia watu mbalimbali ambao wanakuwa wakisumbuliwa
na tatizo la kuchajia simu zao pale ambapo panakuwa hakuna umeme wa
uhakika"alisema Meck Mbwana ambaye ni mvumbuzi na mkurugenzi mtendaji wa
PUKU.
Aliongeza kuwa " kumekuwa na
ongezeko kubwa la matumizi ya simu za smart phone huku watumiaji wakilalama
kuwa wanakosa uhakika wa umeme wa kuzihudumia sasa hii bidhaa itasaidia".
Aliongeza kuwa kwa sasa zinapatikana
hapa nchini na aliwataja wahusika wakubwa kuwa ni pamoja na Ed Kavishe-mshirika
mwenza, Joseph sikare – Rais Tanzania huku Mwanamitindo Millen Magese akiwa ni mshirika
mwenza na balozi wao.
Kwa upande wake Millen aliwataka
wananchi kutumia bidhaa hiyo kwa kuwa mbali na kuwa ni ubora bali pia ni bidhaa
ya watanzania wenyewe.
Tayari PUKU wameshajikita na
uchangiaji wa huduma kwa jamii ambapo asilimia kadhaa ya mauzo itaelekezwa
kwenye kampeni ya uelewa wa hali ya endometriosis na ujenzi wa hospital kwa
ajili ya magonjwa yanayowasumbua akina mama. Mbali na udhamini wa kampeni ya
endometriosis PUKU watachangia ujenzi wa madarasa mawili yaliyoko chini ya
mradi wa Millen Magese Foundation yanayojengwa huko Mtwara ambapo mpaka sasa
madarasa matatu yameshakamilika.
Mwisho.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni