Zinazobamba

Wanachama wa Yanga ‘wamgwaya’ Yusuph Manj Yeye mweyewe ajikataai

Lile sakata la wanachama wa clabu ya Yanga waliokuwa wanapinga maamuzi ya mkutano mkuu wa clabu hiyo wa kumuongezea muda mwenyekiti huyo sasa limefika mwisho baada ya msemaji wa klabu hiyo kuufunga rasmi mjadala huo
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, afisa habari wa klabu hiyo kongwe hapa nchini, Bw. Baraka Kizuguto amesema mjadala ambao ulikuwa umeibuliwa na wanachama wasiofahamika sasa tumeufunga rasmi kwani tuliwapa fulsa ya wao kujitokeza ili tujue hoja zao kwa kipindi cha wingi nzima lakini ndani ya mudahuo hakuna mwanachama yeyote aliyethubutu kuja katika klabu kuelezea kero zao,
yusuf manji

Tuliamua kulitatua tatizo hilo ambalo limeibuliwa na wanachama wasiofahamika kwa kuweka daftari la kuwaandikisha wanachama hao ili tulinganishe wingi wao na wale ambao wametoa maamuzi kule polisi officer mess"

Mpaka kufikia jana majira saa 10:30 jana jioni ni mwanachama mmoja tu ambaye ni Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji, ndiye pekee aliyejiandikisha katika daftari la maalumu la kupinga maamuzi ya mkutano mkuu uliofanyika hivi karibuni.

Mjadala sasa tumefunga rasmi kwani wakati uliobaki sasa ni wa kufanya kazi, 


Hakuna maoni