Zinazobamba

STIPRO: YAANIKA MIKAKATI YAKE YA MIAKA MITANO IJAYO, NI KUHUSU TAFITI ZA KISAYANSI NA JINSI ZINAVYOWEZA KUMKOMBOA MTANZANIA


Mkurugenzi mtendaji wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya STIPRO Prof. Bitrina D. Diyamett (PHD) akifafanua jambo mbele ya mwandishi wa habari wa mtandao huu mapema hii leo. Prof. Diyamett amesema asai yake imedhamilia kufanya tafiti na kuandaa sera zitakazoleta majibu ya matatizo yetu ya msingi.
Asasi isiyokuwa ya kiserikali STIPRO leo hii imeanika mipango kazi yake kwa miaka mitano ijayo kwa wadau, ili kuona ni namna gani watakavyoweza kuisaidia jamii kwa kupitia tafiti za kisayansi kuwakwamua kiuchumi,

Akizungumza na mwandishi wa habari wa mtandao huu, mapema hii leo katika mahojiano maalum, Prof.Bitrina Diayamett amekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika jamii ya kitanzania hususani katika sekta ya viwanda ambapo kwa muda mrefu viwanda vyetu vimekuwa vikazalisha bidhaa zake kwa gharama za hali ya juu hivyo kumlisha mteja wake kwa bei ya juu sana,

Amesema ili kuondoa tatizo hilo, Asasi yake imeamua kufanya tafiti za kisayansi kujua hasa tatizo ni nini? mpaka viwanda vyetu vinadhalisha kwa hasara na nini kifanyike ili kuondoa tatizo hilo,
Diyamett amesema tukifanikiwa kuondoa kiini cha tatizo katika viwanda vyetu hakika hata bei za vyakula vitashuka na hivyo kumpunguzia mzigo mtanzania ambaye mpaka leo bado anamzigo mkubwa wa bei za bidhaa hata nchini.,
"Ndugu mwandishi hapa Tanzania tuna shida moja nayo ni kufanya tafiti zetu ili zitukomboe wenyewe, wengi wao wanafanya tafiti kwa kukopi za watu ambazo hazina tija kwa mtanzania sasa asai hii imejikita kuondoa matatizo hayo pamoja na kuandaa sera zitakazo leta tija kwa mtanzania mmojammoja|Aliongeza Diyamett


Diyamett akifafanua jambo kwa wadau ambao kuhusiana na asasi yake na jitihada watakazo chukua katika miaka mitano mingine, Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Diyamett amekili kufurahishwa na utendaji kazi wa kampuni yake kwani sera mbalimbali zilizofanyiwa utafiti wa kisayansi na asasi hiyo ziliweza kutumiwa na serikali katika kufanya utekelezaji wake.
Wadau katika mkutano huo wa mpango mkakati wa asasi ya STIPRO wakifuatilia kwa makini hoja iliyokuwa ikiwasilishwa na mkurugenzi wa asasi hiyo, B. Bitrina Diyamett.

Hakuna maoni