Zinazobamba

HABARI ILIYOTIKISA JIJI: SHIRIKA LA VIWANGO DUNIANI LAITUZA TUZO TCRA, NKOMA ASEMA HAWATABWETEKA KAMWE


Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya mawasiiano Prof. John Nkoma akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu cheti walichopewa kama ishara ya kuona jitihada zao wanazofanya katika kuhakikisha sekta ya mawasiliano hapa nchini hayamnafaishi mwkezaji peke yake bali hata mtumiaji wa huduma hiyo anufaike. Tuzo hiyo inadumu kwa kipindi cha miaka mitatu na kama hawatafanya juhudi za kuongeza ufanisi wa kazi basi tuzo hiyo itawaponyoka.
 Shirika la Viwango Duniani limekadhi Cheti kwa  mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA)  baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa taasisi hiyo ya serikali chini ya Mkurugenzi wake Prof. John Nkoma
 
  Cheti  hicho kilikabidhiwa jijini Dar es Salaam leo, mbele ya wafanyakazi wote wa TCRA na Mkaguzi wa kimataifa kutoka Uingereza Andrew Rowe na kumpa Mkurugenzi wa TCRA Prof. John Mkoma.
 
Akikabidhi cheti hicho, mkaguzi huyo wa kimataifa toka Nchini Uingeleza Bw. Andrew Rowe, Aliitaka TCRA kuhakikisha wanapigania katika utoaji wa huduma bora ili kuendelea kubaki na cheti hicho kinachowatambulisha kimataifa.
 “Mnatakiwa kuongeza juhudi katika utoaji wa huduma ya mawasiliano kwani ni sekta muhimu kwa taifa hasa Tanzania” alitoa rai Andrew.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA, Prof. John Nkoma, amesema kuwa mafanikio hayo yalioonekana na shirika la viwango Duniani hayakuja kama miujiza bali kuna kazi kubwa imefanywa na ndio maana wenzetu wa viwango wameona kazi hiyo na kuja kutupongeza,
" utendaji wetu kazi mzuri ndani ya mamlaka hii katika kudhibiti mawasiliano nchini, ndio sababu iliyopelekea kupata cheti hiki kinachoipa heshima Tanzania." Alisema Prof. Nkoma
Profesa Nkoma, alieleza kuwa umefikia wakati muhafaka wa sekta hiyo kufanya kazi kwa ufanisi ifikapo 2017 ili Shirika hilo litakapokuja kufanya ukaguzi wakute utendaji kazi upo juu.
     “Cheti tulichopata ni ISO 900:2008  kimetokana na ushirikiano tulionao miongoni mwa wafanyakazi wote na sio mkurugenzi peke yake, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutetea cheti hiki ambacho kinadumu hadi mwaka 2017,” alisema Prof. Mkoma. 

Akizungumzia ubora wa cheti hicho, Mhandisi  kutoka Shirika la Viwango Tanzania  (TBS), Salvatory Rusimbi, alisema kutokana na viwango bora vya kazi, uongozi bora na matumizi bora ya rasilimali zinazo tumika kunufaisha utendaji kazi ndio vitu vilivyochangia kupata cheti hicho.
 
 “Naipongeza TCRA kwani mkaguzi ameona kazi inayofanywa katika utoaji wa mawasiliano nchini pia utendaji huu utawanufaisha wateja hivyo inatakiwa kuongeza ushirikiano katika kazi” alisema Rusimbi.


Hakuna maoni