IDARA YA USALAMA LAWAMANI,WASHINDWA KUMCHUKULIA HATUA JAMBAZI LINALOTIKISA JIJI AMBALO LINATOKA NCHINI NIGERIA SOMA HAPA KWA KINA
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa Rashidi Othoman picha na Maktaba
Na Karoli Vinsent
IDARA ya Usalama wa Taifa umeingia
kwenye shutuma nzito kutokana kitendo chake cha kushindwa kumthibiti,Jambazi
mwenye uraia wa Nigeria ambaye amekuwa akifanya Uharifu huku, Jambazi huyo akijinadi
kwamba hakuna wakuchukulia hatua hapa nchini,Mtandao huu umebaini.
Jambazi, huyo,ambaye anajulikana kwa jina Kingsley O.Ugiagble ambae
amekuwa akifanya ujambazi ndani ya nchi pamoja na kumiliki mtambo wa
kutengeneza Fedha za Kimarekani “Dola” pamoja na za Ndani vilevile kufanya wizi
kwenye Hudama za Benki ATM
.
.
Uchunguzi, uliofanywa na Mwandishi wa Mtandao huu umebaini Jambazi huyo
mwenye Asiri ya Nigeria ambaye anakaa Maeneo mbezi jijini Dar es Salaam,kwenye
nyumba ambayo yenye Thamani ya milioni 250,jambazi huyo amekuwa akihusika na
mtandao wa kutenganeza fedha feki za kimarekani yaani Dora.
Chanzo hicho cha Habari kilizidi kusema Kingsley amekuwa amekuwa
anahusika kuleta Silaha ambazo zimekuwa zikitumika katika Vitendo vya Ujambazi
hapa nchini,huku mamlaka zikishindwa kumchukulia hatua.
Kingsley ambae amekuwa akijinadi kwamba hakuna wa kumchukulia hatua
kutokana kujuana na Wataendaji wakubwa ndani ya Idara nyeti ya Usalama wa
Taifa,hatahivyo chanzo hicho cha Habari kilimtaja jamabazi huyo kuhusika kumiliki
mitambo miwili ya Kutengeneza Fedha Bandia ambayo hutumika kutengeneza noti ya
sh 10000.
Ambapo mtambo mwengine unatengeneza Dola za Kimarekani ambazo sio rahisi
kuzitambua.Taarifahiyo inasema fedha hizo zipo kwenye mzunguko wa Fedha kwa
maana zikipitishwa kwenye utambuzi maramoja ni vigumu kuzitambua mpaka
utakaporudia marambili ndipo mashine hiyo utambuzi itagoma.
Uchunguzi wa Mwandishi wa Mtandao huu amebani Mtambo huo wa
kutengeneza Fedha hizo bandia unahifadhiwa katika nyumba moja maeneo ya Kunduchi
jijini Dar es Salaam na kuendelea na mpango wake wa Kudurufu Fedha hizo huku
Idara za Usalama zikimwogopa Jambazi huyo.
Kingsley,ambaye ameingia nchini kutoka nchini Nigeria pasipokuwa na
Pasipoti za Nchini tena wala bila hata fedha yeyote ambapo amekuwa akipata
fedha nyingi kutokana na hujuma hiyo anayofanya ndani ya nchi kutokana vitendo
hivyo vya kijambazi.
Kwa mujibu wa Vyanzo vya kuamika zinasema Jambazi Kingsley kabla ya kuja
nchini aliwai kufanya vitendo hivyo vya Ujambazi katika Nchi za Ghana,Kenya
pamoja na Nigeria,ambapo hivi sasa amehamina nchini na kuendelea na vitendo
hivyo.
Akilizungumia hili Kigogo kutoka ndani Idara ya Usalama na ulinzi wa
Taifa ambae akuta Jina lake liandikwe mtandaoni kwa kusema yeye sio msemaji wa
Idara hiyo alisema mtandao wa Jambazi huyo ambae ni raia wa Nigeria ni mkubwa
sana.
“Sikufichi mwandishi,huyo Jambazi
mtandao wake ni mkubwa sana ndio maana hata sisi kumchukulia hatua tunasuasua
tu,kwasababu marayakwanza alikamatwa na kufika hatua ya kumrudisha kwao Nigeria
lakini sisi wenyewe tiligeukana tukamlejesha
tena”alisema mpashaji huyo wa taarifa.
Duru hizo
zinasema Jeuri anayoionyesha Kingsley,inatokana na kuwa na uwezo wa juu
kifedha ndio maana kushindwa kuchukuliwa hatua,kwani Vyombo vya Habari vimekuwa
vikifichua vitendo vyake huku mamlaka zikisuasua kumchukulia hatua
Hakuna maoni
Chapisha Maoni