MSAKA URAIS WAZIRI MEMBE,AZIDI KUWAPUUZA VIONGOZI WA JUU WA CCM,SASA AZIDISHA HARAKATI ZAKE ZA KUTAKA URAIS
Pichani Bernard Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (picha ya Maktaba)
Na Karoli Vinsent
WASAKA urais ndani ya chama cha
Mapinduzi CCM waanza kukipasua chama hicho,kutokana na Hivi sasa chama hicho
kuanza kumwogopa Waziri Bernardi Membe,mtandao huu umedokezwa.
Mhe. Bernard K. Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ameonekana kuwa na nguvu ndani
ya chama hicho kutokana na kitendo chake kuendelea kufanya Kampeni za
chinichini katika mbio za kusaka urais mwakani 2015, ambapo amekuwa amevunja
kanuni za chama hicho.
Mapema mwezi februari,mwaka huu
Kamati maalum ya maadili ya chama cha mapinduzi CCM ,ambayo iliwahoji vigogo
sita wa chama hicho tawala ambao walikuwa wanaonekana maeneo mbalimbali
wakiendeleza harakati za kumrithi Jakaya Kikwete ambae anatarajiwa kuondoka
mwakani 2015.
Lakini kamati hiyo ya maadili ya chama
iliwafungia kwa mda wa mwaka mmoja makada sita wa chama hicho kutofanya
harakati zozote za kusaka urais ndani ya chama hicho makada hao ni Waziri
aliyejiuzulu Edward Lowassa,Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa
Berdanard Membe,waziri Mkuu wa awamu ya tatu Fredrick sumaye.
Mbali na hao wengine ni Waziri wa
ushirikiano wa Africa mashariki Samweli Sitta,Mbunge wa Sengerema Wiliam
Ngeleja,waziri Stephen Wasira pamoja na Naibu waziri wa mawasiliano,sayansi na
Tekolojia January Makamba.
Licha ya Kamati ya chama hicho
kuwafungia makada hao kwa miezi 12,lakini Waziri Membe,ameonyesha kupuuza maamuzi
ya chama hicho kutokana na kuanza harakati za kusaka urais huku viongozi wa
chama hicho,akiwemo mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete kulinyamazia Suala
hilo.Membe amekuwa akipambana kwa hari na mali kuhakikisha anakamata nafasi
hiyo ya juu ya uongozi wa Taifa hili.
Waziri Membe alianza kuonyesha kupuuza
kauli hiyo Wiki iliyopita alipokuwa anazindua Filamu ya Love of Mwanza ambapo
alitumia nafasi hiyo kujitangaza Kisiasa,huku akitumia Kifua cha Rais Jakaya
Kikwete kupuuza Adhabu ya Kamati maadili ya chama cha mapinduzi,ambayo
walimzuia kufanya hivyo.
Membe alionekana kulitumia Jina la
Jakaya Kikwete kama njia ya kuwaogopesha Wasaka Urais wenzake ambao wamekuwa
wakiwakimya kwa sasa,ambapo alisema alichokifanya hapo kimetokana na kupewa
Baraka na Rais jakaya Kiwete ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM
aliyekuwa Juu wajumbe waliotua hukumu hiyo.
“Nilikutana na Rais Kikwete Juzi kumuaga na kumueleza ujio wangu Jijini
Mwanza kuwa nimeitwa na wasanii wa Filamu naye alikubalia na kunitaka nifanya
haraka na nisiache baada ya kurudi Jijini Dar esSalaam nikampatie taarifa za
kile nilichokishuhudia Jijini Mwanza,hivyo nimekuja na Marafiki zangu ambao ni
Frends of Membe”alisema Membe.
Achia mbali uzinduzi huo wa Filamu
mkoani mwanza,Waziri membe akafanya harakati zengine ambazo zinatafsiriwa kama
ni Harakati za kusaka urais baada ya kuandaa Semina ya Siku saba kwa Umoja wa
Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM, iliyofanyika ukumbi wa Msasani Club,Jijini
Dar es Salaam,ambapo katika semina ambayo iliandaliwa na Kufadhiliwa na Waziri
Membe.
Katika Semina hiyo ilivaa koti la nje
kwamba ilikuwa inawapa vijana wa CCM uwezo wa kuwajengea ili waweze kupambana
Na Umoja wa Katiba yaWananchi UKAWA,lakini mambo yalikuwa sivyo kutokana na
Semina hiyo ilionekana kama njia ya Waziri Membe kujinadi katika kusaka urais.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika
zinasema Waziri Membe alitoa zaidi ya Milioni 200,ili kugalimu Semina
hiyo,katika kufanikisha ambapo wajumbe walipata Posho pamoja na chukula,
Kufanya usaliti huu kwa Waziri Membe,inatafsiliwa kama ni kuingia
mpasuko ndani chama hicho Kikongwe barani Afrika ambacho kipo
madarakani,kutokana na Maamuzi waliyofikia ya kuwafungia makada hao.
Akilizungumzia hili,Mjumbe wa
Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM, kutoka mikoa ya kusini,ambaye
hakutaka jina lake litajwe kwenye Mtandao huu,alisema ni wazi chama hicho
kinamwogopa Waziri Membe.
”Mimi mwenyewe nashangaa sana
huyu Msaka urais waziri membe anavyoogopwa namna hii ndani ya chama
chetu,kwani ukweli huko wazi huyu anatumia ukaribu wake alikuwa nao kwa Rais
kikwete,ndio unamfanya kuzidisha kufanya harakati za kusaka urais,lakini
kwanini wasimpe adhabu kari huyu msaka urais”
“Kama wanaona wameshindwa kuwazuia ni
bora waache waendelee na harakati zao tu maana wengine tunawatu wetu tunataka
tuwasapoti tu na waruhusu tushindane tu”alisema mpashaji huyo wa Taarifa.
Kuonyesha huku jeuri kwa Waziri Membe,
kumekuja ikiwa Miezi miene kupita baada kamati ya Maadili ya chama hicho
kuwafungia makada hao.
Ambapo chama hicho kilifuata kanuni
ambapo ibara 6 (2) (1_5) ya maadili ya Viongozi wa Chama hicho inawazuia kutoa
mchango,misaada zawadi za aina yeyote,kukusanya michango na kufanya kampeni
bila ya kupata kibali kutoka kamati ya Siasa ya Halmashauri ya eneo husika.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni