TAARIFA MUHIMU TOKA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DARESAALAM LEO HII,
KOVA AKIFAFANUA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI |
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI
LA POLISI TANZANIA
PRESS
RELEASE
01/07/2014
JESHI
LA POLISI LAWASHIKILIA MAJAMBAZI SUGU 8 KWA TUHUMA MBALIMBALI ZA
UJAMBAZI.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata majambazi sugu
wanane ambao wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ya ujambazi jijini
Dar es Salaam. Katika uhalifu huu majambazi hao walisababisha vifo,
majeraha, wizi wa mali na fedha taslimu. Katika matukio hayo
walitumia silaha za moto ikiwa ni paoja na bunduki aina ya SMG,
Bastola na vifaa mbalimbali vya uvunjaji ikiwa ni pamoja na baruti.
Majambazi
hao wamekamatwa kutopkana na oparesheni kali inayoendelea jijini Dar
es Salaam baada ya kifo cha Mtawa wa Kanisa Katoriki Sista CLESENCIA
D/O KAPURI, Miaka 50, Mhasibu wa Parokia ya Makoka, kilichotokea
tarehe 23/06/2014 eneo l Ubungo Kibangu.
Wawili
kati ya watuhumiwa hao nane, wamehusishwa moja kwa moja na tukio la
kuuawa kwa Mtawa huyo ambao wa kwanza ni MANASE S/OGENYEKA @ MJESHI,
miaka 35, Mkazi wa Tabata Chang’ombe, ambaye pia ni mwendesha
bodaboda. Wa pili ni HAMIS S/O ISMAIL, SHABAN @ CARLOS,
Mfanyabiashara, Mkazi wa Magomeni Mwembechai.
Majambazi
hawa wawili hatari licha ya kuhusishwa na tukio la kifo cha Mtawa na
kupora million ishirini (20,000,000/=), pia walikuwa wakitafutwa kwa
muda mrefu kwa tuhuma za tukio la uporaji wa Benki ya BARCRAYS tawi
la Kinindoni lililotokea tarehe …………………. Ambapo
mamillioni ya fedha yaliibwa kabla na baada ya tukio la uporaji.
Jambazi MANASE S/OGENYEKA @ MJESHI, ndiye aliyeendesha pikipiki
akimbeba jambazi mwenzake akiwa na fuko la mamillioni ya fedha na
kutoroka nazo wakati ambapo jambazi HAMIS S/O ISMAIL, SHABAN @
CARLOS, ndiye aliyekuwa kiongozi katika tukio hilo.
Jeshi
la Polisi bado linawatafuta watuhumiwa wengine wawili katika tukio la
Mtawa na jambazi mmoja kwa jina maarufu la LEONARD S/O MOLLEL katika
tukio la Barcrays Bank ambaye alitangazwa na kisha picha zake kutolwa
katika vyombo mbalimbali vua habari.
Majambazi
hao wawili pia wameshirikiana na wenzao sita kama ifuatavyo:
- BEDA S/O MALLYA, Miaka 37, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbezi Msakuzi.
- MICHAEL S/O ROMAN MUSHI @ MASAWE, Miaka 50, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbezi Makabe – Kimara.
- SADICK S/O MOHAMED KISIA, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbagala Kizuiani.
- ELIBARIKI S/O ELIAH MAKUMBA, Miaka 30, Mkazi wa Buguruni Madenge.
- NURDINI S/O SULEIMAN, Miaka 40, Mkazi wa Buguruni Madenge.
- MRUMI S/O HAMAD SALEHE @ Chai Bora, Miaka 38, Mkazi wa Kigogo Fresh.
Licha
ya kushiriki katika matukio mbalimbali watuhumiwa hawa watatu
ELIBARIKI S/O ELIAH MAKUMBA, NURDINI S/O SULEIMAN, na MRUMI S/O HAMAD
SALEHE @ Chai Bora, walikamatwa baada ya kutumia mbinu ya hati bandia
wakiwa wananomba kazi katika kampuni binafsi ya ulinzi iitwayo
“INSTANT SECURITY SERVICES” iliyopo mtaa wa Msasani Makangira.
Majambazi hawa walikuwa wanaomba kazi ya ulinzi katika kampuni hiyo
ili baadye waweze kutenda uhalifu wao wenyewe au wawaruhusu
wanamtandao wenzao waweze kutenda uhalifu kwa urahisi.
TAHADHARI
KWA MAKAMPUNI YA ULINZI
Kutokana
na mtindi uliozuka hivi karibuni wa majambazi kuomba kazi na baadaye
kuwaruhusu wenzao kuiba katika kampuni hizo, tunatoa tahadhari kwa
makampuni binafsi ya ulinzi kwamba wanapotaka kuajiri washirikiane
moja kwa moja na Jeshi la Polisi ili wafanye upekuzi wa pamoja
(VETING) utakaohusisha alama za vidole, picha, na ukaguzi wa
kumbukumbu muhimu za kibayologia kama vile vipimo vya DNA na
kadhalika.
Upelelezi
wa mashauri mbalimbali yanayowahusu majambazi hawa unaendelea na
hatimaye majalada ya kesi yatapelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali
kabla ya kupelekwa Mahakamani.
SULEIMAN
H. KOVA
KAMISHNA
WA POLISI KANDA MAALUM
DAR
ES SALAAM.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni