MAMA SALMA KIKWETE LAWAMANI,ASASI YAKE YAGEUKA NI YA WAKE WA VIGOGO WA CCM.SOMA HAPA KWA MAKINI, UONE JINSI WALIVYOPEANA MADARAKA
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (picha na Maktaba) |
RAFU mbaya za Kisiasa zilizofanywa
na Chama cha Mapinduzi CCM ndani ya Asasi inayohusu Masuala ya Maendeleo na
kuwajengea uwezo( WAMA),Zazidi kuiweka Asasi hiyo Njia panda,Mtandao huu
imedokezwa.
Asasi hii ambayo ilianzishwa mara
tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia Madarakani mwaka 2005 na kupewa jina la
wanawake na Maendeleo WAMA,na kutambulishwa kupitia jina la mke wa Rais
Kikwete,Mama Salma Kikwete.
Uchunguzi uliofanywa na Mtandao huu umebaini asasi hiyo imegeuka ya Wake
wa Vigogo kutoka Ndani chama cha Mapinduzi,CCM na kugeuka kuwa miongoni mwa
asasi inayofanya kazi ya kuwaingiza madarakani Vigogo hao,huku ni kinyume
na Matarajio ya wengi kwenye Asasi hiyo.
Kwa mujibu wa sheria inayosimamia Asasi zisizo za Kiserikali nchini
zinazuiliwa kwa Asasi kujiingiza katika masuala ya Kisiasa,lakini kwa asasi hii
ya WAMA,inaonekana wazi kwenda kinyume kutokana kufanya kampeni ya Mgombea wa
Urais mwaka 2010 kupitia CCM.
Asasi hii imekuwa ikipigiwa kelele na Wabunge kutoka vyama upinzani
nchini kwa kuishutumu kugeuka kuwa asasi ya chama cha Mapinduzi CCM.
Kwa mujibu wa Vyanzo vya kuaminika ambavyo mwandishi wa Mtandao huu
ameziona, zinaonyesha Jinsi Rafu ilivyofanyika katika Asasi hiyo kutokana
Wajumbe wa Juu kwenye umoja huo wa Wanawake nchini,ambao ni Wake wa Viongozi na
Makada kutoka CCM.
Chanzo hicho kilionyesha kuwa, Mwenyekiti wa Asasi hiyo ni mke wa Rais
Kikwete,mama Salma Kikwete,ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM
(NEC-CC)kutoka mkoa wa Lindi,
Chanzo hicho pia kilimtaja Mjumbe wa Pili ambae ni Zakhia Meghji,huyu
ambae ni mweka hazina Mkuu wa CCM na Mjumbe wa Kamati kuu cha hicho tawala
ambacho ni chama pekee kikongwe ambacho kipo madalakani kusini mwa Jangwa la
Sahara.
Vilevile Meghji,amepewa ulaji mwengine na Serikali yake ya CCM na kwa
kuchaguliwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumbe la Taifa NHC.
Mjumbe
mwengine wa Tatu,Mwanamwema Shein,mke wa Dk Ali Muhamedi Shein ambaye ni Rais
wa Zanzibar na Makamo Mwenyekiti wa CCM
Chanzo hicho kilizidi kutaja hujuma pamoja na Rafu inayofanywa na chama
cha Mapinduzi kwenye Asasi hiyo kwa kumtaja Mjumbe wa Nne,ambaye Sophia
Simba.Huyu ni Mwenyekiti wa Ummoja wa Wanawake wa CCM (UWT-CCM) .
Sophia Simba,ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii,wanawake na
Watoto.ambapo kisheria anapaswa kusimamia asasi zifuate maadili lakini
ameshindwa kabisa kuisiamia Asasi ya Wama ambayo imekuwa ikijiingiza kisiasa.
Mjumbe mwengine ni Regina Lowassa,mke wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu
mwaka 2007 kwa shinikizo la Bunge kufuatia kuhusika na ufisadi na Kashfa ya Mkataba
wa Richmoond.
Mume wa Regina vilevile ni Mbunge wa Munduli,ni mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Bunge la Tanzania,mbaye ni pia ni miongoni mwa watu
wanaotumia kila aina ya njia kuhakikisha anakuwa Rais 2015.
Rafu hii ilizidi kujidhilisha baada ya kubainika Mjumbe mwengine ambaye
ni Blandina Nyoni kuwepo kwenye Bodi ya Wama.mama huyu aliwai kuwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya ambapo alisimamishwa kutokana kuzidisha ukilitimba ofisini.
Duru zinasema Asasi hiyo,ambao iliazishwa kuwatetea wanawake kwa
kuwaondoa kwenye lindi la Umasikini kwa kutoangalia upande wowote wa chama,
lakini kwa sasa imeguka kuwa ni Asasi ya kuwaingiza wajumbe hao pamoja na
wanaume zao kubaki Kula neema ya nchi kuliko kuwatetea wanawake.
Kwa upande wake Mchambuzi wa Kisiasa na
Msomi pia wa Masuala ya kisiasa kutoka chuo Kikuu cha Dodoma Seiph Yahaya
alisema Hakuna Jipya kwenye asasi hiyo,na ipo kwa manufaa ya Tabaka Tawala tu.
“Sikiliza nikwambie,hapo hakuna
kitu, tu hapo ni mpango wa kuhakisha wake waViongozi wanazidi kuneimeka
tu,kwani kama Asasi hiyo ingekuwa inania Nzuri kwanini hakuna hata mjumbe
yeyote kwenye bodi hiyo kutoka Chadema wala Cuf”
“Huu ni mwendelezo wa kutudanganya
watanzania kwasabu washatujua sisi mazezeta sana,na hata mimi namshangaa sana
waziri Sophia Simba na kushindwa hata kutetea sakata hili”alisema Seiph
Hakuna maoni
Chapisha Maoni