Zinazobamba

BREEKING NEWZZ,LIPUMBA, MAALIM SEIF JUMA DUNI HAJI "WASHINDA KWA KISHINDO" CUF, WADAU WASEMA USLTANI BADO UNAENDELEA HUKO CUF

Kama Ufalme wa Prof.Lipumba ni huu wakupendwa na watu wengi aendelee tuu kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF.Uchaguzi ndo hivyo umemalizika na mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti Prof.Lipumba, ameibuka kidedea huku makam mwenyekiti Mh.Juma Duni Hajjinaye akipigiwa kura za ndio nyingi tu
Aidha katika uchaguzi huu uliomalizika hivi punde wanachama wa CUF wamemlejesha tena katibu mkuu wao Maalim Seif Sharif Hamad kuendelea na kazi nzito ambayo ameianza ya kuhakikisha analeta haki sawa kwa wote.
Wagombea wa uenyekiti wa chama hicho PROFESA IBRAHIMU LIPUMBA akiwa anajadili jambo na mgombea mwezake kabla ya wajumbe kuamua nani wampe tena uenyekiti wa chama hicho cha CUF leo , Katika uchaguzi uliomalizika hivi punde Prof. Lipumba amerudishwa tena madarakani

Katika uchaguzi huo, wagombea mbalimbali wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali Katika nafasi ya uenyekiti wa chama cha CUF taifa wagombea watatu wamejitokeza kugombea nafasi hiyo ambao kwa majina ni aliyekuwa mwenyekiti wake PR. HARUNA LIPUMBA,MH CHIEF Lo TUTAYOSA YEMBA,pamoja na Mh. MBEZI na Adam Balari ambapo kati yao Prof Lipumba ameibuka kidedea 
Katika nafasi ya makamu mwenyekiti na katibu wakijitokeza wagombea mmoja mmoja ambao ni katika umakamu wa mwenyekiti amejitokeza  mh JUM,A DUNI HAJI,na katika nafasi ya katibu mkuu wa chama hicho amejitokeza mh SEIF SHARIF HAMAD ambaye alikuwa ameshikilia nafasi hiyo.
Aliyekuwa katibu mkuu wa CUF  SEIF SHARIF HAMAD akiomba kura kupata nafasi hiyo kwa mara nyingine tena muda huu katika uchaguzi mkuu wa
chama hicho unaoendelea muda huu ndani ya ukumbi wa ubungo plaza jijini dar es salaam. hata hivyo wananchi wamempenda sana na amerejeshewa madaraka yake huko CUF.



Uchaguzi wa kuwapata wawakilishi katika mkutano mkuuu wa chama hichi tayari umemalizika na tayari wajume hawa ndio wajumbe wa mkutano mkuu wa
chama cha wananchi CUF waliochaguliwa muda huu jijini Dar es salaam

Hakuna maoni