Zinazobamba

Waziri Nyarandu tayari kafanya yake, soma hapaa


2 (3)
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akizungumza na hadhiri wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Afrika mwaka 2014 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo



3 (3)Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, akijisajili kushirikia kwenye tovuti ya Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Afrika mwaka 2014, kama ishara ya kuzindua tovuti hiyo, shughuli iliyofanyika  kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maimuna Tarishi na Msemaji wa Wizara Nurdin Chamuya.
“Wengi mnaweza kujiuliza kwa nini tunazindua, ni sahihi jibu kuwa:
moja tunajivunia kwa kuandaa tukio muhimu kwa manufaa ya Afrika nzima katika kuendeleza ufugaji nyuki” alisema Waziri Nyalandu na kuongeza:
“Mbili tunaitangaza Tanzania duniani kote kuwa maliasili tulizonazo yaani misitu na mapori yanatumika kwa kufuga nyuki; tatu Wizara ya Maliasili na Utalii inaandaa kongamano hili ili kuhamasisha ufugaji nyuki nchini”
Waziri Nyalandu alieleza sababu nyingine la kuandaa kongamano hilo ni heshima kwamba Tanzania inawajali wafugaji nyuki kwa kuwa ni kongamano la kwanza kufanyika Afrika na Tanzania.
“Nachukua fursa hii kuwaomba wafugaji nyuki, wataalamu wa fani mbalimbali, watafiti, waandishi wa habari, wafanyabiashara, wanafunzi na watendaji katika taasisi mbalimbali kushiriki kongamano hili” alibainisha Waziri Nyalandu.

1 (3)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri huyo kuzungumza na kuzindua tovuti ya Kongamano la Kwanza la Ufugaji Nyuki Afrika mwaka 2014 uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo Maimuna Tarishi alisema tovuti ya kongamano ambayo ni http://www.apiafrica.org iliandaliwa na kuanza kutumika Februari mwaka 2014.
Aliongeza kuwa tuvuti hiyo inawezesha kupata taarifa muhimu za mahali litakapofanyika, kujiandikisha, kulipia banda la maonesho na ziara ya mafunzo, ambapo hadi sasa takriban washiriki 550 wakiwemo 250 kutoka nje ya nchi.
4 (2)
Baadhi ya washiriki wa uzinduzi huo

Alifafanua kuwa Wizara yake kwa kuzingatia uzoefu ilionao kwa kushiriki maonesho mbalimbali, iliona ni vyema kuandaa kongamano hilo ili kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kutoa mchango wa utafiti, teknolojia na kubadilishana uzoefu katika kuboresha, kutunza na kusimamia makundi ya nyuki kwa uzalishaji wenye wingi na ubora.
Kwa mujibu wa Afisa Nyuki Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Monica Kagya ada ya ushiriki kwa washiriki kutoka Tanzania ni Shilingi 100,000, mwanafunzi  Shilingi 20,000 na mshiriki kutoka nje ya nchi ni Dola 250.

Hakuna maoni