MATUSI, KEBEHI DHIDI YA BABA WA TAIFA MWL. JURIUS KAMBARAGE NYERER SASA YACHUKUA SURA MPYA
| Makongoro akiwa mwenye nyuso za furaha baada ya kupokea ugeni huo toka kwa umoja wa vijana wa ccm. |
| Baada ya kuwapokea alipata fursa ya kuwaingiza ndani ili waseme walitaka kusema kwa bibi yao |
| Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Daresalaam akitoa salam zake kwa wenyeji nyumbani kwa mjane, mama Maria nyerere |
| Umoja huo ulikuja na miti ili kupanda katika mashamba yaliyo ndani mwa nyumba ya mama Maria nyerere, Huyu ni mmoja aliyebeba miti hiyo |
| Makongoro Nyerere akiwa sambamba na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere alipoenda kumtoa ndani ili azungumze na wajukuu zake waliomtembela nyumbani kwake. |
| Makongoro Nyerere akishiriki zoezi la upandaji miti kwa niaba ya Bibi, mama Maria nyerere. |
Umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) tamko lao la kuulaani vitendo
viovu vya baadhi ya watu kumtuhumu, kumkebehi na kumtukana baba wa taifa , Mwl.
Jurius Kambarage Nyerere mapema hii leo nyumbani kwa mjane Mama Maria Nyerer,
Tamko hilo limekuja kufuatia kampeni kambambe ambazo
zinaendeshwa na wapinga amani na wale wanaojifanya hawaoni kazi nzuri
iliyofanywa na Baba wa taifa, ambao hivi karibuni wamekuwa wakinukuliwa wakitoa
maneneo ya kashifa dhidi ya Baba wa Taifa,,
Akizungumza nyumbani kwa mjane Mama Maria nyerer, Kiongozi
wa Jumuiko la Vijana wazalendo, na mwenyekiti wa vijana mkoa wa Pwani, Bw.
Mohammedi Nyumbo,amesema kumekuwepo na kampeni yenye nia ovu iliyoasisiwa hivi
karibuni ya kuharibu taswira na heshima ya baba wa taifa katika jamii ya
kitanzania na kimataifa.,
Amesema kampeni hiyo inayoendeshwa na vibaraka wan chi za
magharibi na ulaya, Wazandiki na maadui wa amani ya Tanzania imeendelea
kusambaa kwa kasi na kwa gharama kubwa, hatua inayonyesha kuharikisha mchakato wa kuharibu taswira ya baba wa taifa,
Amesema kwa kutambua mchango wa baba wa taifa kama muasisi
wa taifa hili,mpigania uhuru shupavu, shujaa aliyekuwa na mapenzi ya dhati na taifa lake, umoja huo umeamua
kuukumbusha umma wa kitanzania juu ya
mchango uliotukuka wa baba wa taifa
katika taifa hili na kuhamasisha vijana kuenzi
kwa vitendo moyo wa kujituma, weledi na busara za mwalimu ili kuweza
kuwa na taifa lenye misingi ya kuheshimu
wazee wetu.
Aidha katika hatua nyingine Umoja huo wa vijana
umesikitishwa na vitendo vya bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanznaia kugeuka
kuwa uwanja wa matusi wa kumtukana baba wa Taifa, hakika imewafedhehesha sana,
Nazani imefika wakati sasa kwa bunge tukufu la Tanzania,
kudhibiti na kuondoa kinga yake kwa wale wote ambao kwa ujinga na kutumika
wameamua kuanzisha kuendesha kampeni ya
kutia doa taswira ya BABA wa taifa hili tukufu
No comments
Post a Comment