Zinazobamba

TAN TRADE YAZINDUA MAONYESHO TENA,SASA KAZI KWAKO



        
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade),Jacqueline Mneney Maleko.(picha na Maktaba)

Na Karoli Vinsent
       Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  katika kuanzimisha Siku ya Uhuru wa Afrika, Imeandaa onenyesho kubwa litakalowafanya Watanzania Wafurahia Siku Hiyo.
       Hayo,Yamesemwa Leo Jijini Dar Es Salaam Na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade),Jacqueline Mneney Maleko,wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo alisema Lengo la Tamasha hilo ni kuwashirikisha Wadau Mbalimbali ambao wanatoa Mchango  mkubwa Hapa Nchini.
       “Lengo la Mashindano ni kuwashirikisha Wadau mbalimbali wakiwemo,BASATA,shirikisho  Firamu pamoja na Michezo ya Jadi na Wajasiriamali wadogowadogo,Madhumuni makubwa ya kufanya maonyesho ni kutangaza Ubora wa Bidhaa Zetu”
    “Maana katika Kipindi Cha Miaka Mitano ambacho tumefanya Maonyesho haya,  tumepata muitikio mkubwa kutoka kwa Wajasiriamali,na sasa Tutazidi kutengenezea fursa Ubora wa Bidhaa zetu za Ndani”alisema Mama Maleleko
        Mama Maleleko,alizidi kusema Licha ya Maonyesho haya kufanyika Mfurulizo kwa Miaka Mitano,yametoa mwanya kwa Wajisiriamali wa Ndani kujitangaza na kuwataka Wananchi wajitokeze kwa Wingi kuja kushuhudia Maonyesho haya yatakayofanyika Tarehe 20  hadi tarehe 25 mwezi huu Viwanja vya Mnazi Mmja Jijini Dar Es Salaam.
         Mamlaka hiyo ambayo imekuwa ukisimamia Maonyesho yanojulika kama Sabasaba.ilisema ,Maonyesho hayo yatashirikisha Zaidi ya Mikoa ya 14 ya Tanzania Bara Pamoja Zanzazibar.
        Mgen,i Rasmi katika Maonyesho hayo,atakuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara,na pia yatakuwepo Mashirika ya Rafiki kama TFDA na mengineyo kwa Lengo la kuwapa wajasiliamali Fursa ya kufahamu ubora wa Bidhaa zao

No comments