MAMA MARIA NYERERE ATOA WOSIA MKALI KWA WATANZANIA, ASIMULIA USIYAJUA, ADAI BABA WA TAIFA KAMTOKEA KWENYE KITI CHA ENZI NA KUMTAKA ASEME YOTE,
Mjane wa Baba wa taifa la Tanzania, Mama Maria nyerere Amewataka watanzania kuchukua hatua za haraka za kuondoa matabaka ambayo sasa yanaenea kwa kasi kubwa kwani wasipochukua tahadhali mapema kuna hatari ya kutokea vita kubwa ambayo itasambaratisha taifa,
Akizungumza na wajukuu zake mapema hii leo, Bibi huyo amesema ameamua kufunguka baada ya baba wa taifa kumtokea katika chozi na kumtaka kusema mapema yale yote anayoyajua vinginevyo taifa likiingia kwenye vita, siku ya kufika mbele ya haki atamuuliza ni kwa nini hajasema ukweli kwa watanzania ili taifa likanusurika na vita ambayo itasambaratisha taifa,|
" Chokochoko hizi zinazofanywa na watu wenyenia ovu ya kuharibu taswira ya
baba wa taifa hakika imenifedhehesha ingawaje nafahamu, matusi kama haya
yalifanyika pale misri na matokeo yakw ni vita ambayo mpaka leo bado
inawagharimu Alisema mama Maria Nyerere"
Maria ameendelea kufunguka kuwa matusi, kebehi na lugha chafu zinazotolewa na viongzi wa kutumainiwa hapa nchini si makosa yao na kusema kuwa hali hiyo inatokana na vitendo vya kumkosea mungu na kwamba dawa pekee ambayo watanzanania wanatakiwa kuichukua ni kuomba na kusali ili taifa lisiingie katika vita ambayo itaharibu misngi mizuri ambayo iliwahi kuwekwa na waasisi wetu wa taifa,
Maria amesema si kweli kwamba enzi za nyerere watu walikuwa hawambishii, au wakatofautiana kimaneno lakini, hali ilivyo sasa, inatia shaka kwani matusi mengi yamekuwa yakienea kila siku huku hatua dhidi ya wanaohusika kutochukuliwa na kuacha wakitembea kifua mbele,
Amesema, hatua ya binadam kutusi waasisi wao haijaanzia hapa kwetu bali imeanzia mbali sana, Angalia nchi kama Misri Libya zote hizo ni mifano mizuri ambayo watu wake wamekuwa wakitukana wazee wao na kusihia katika vita ambayo inawagharimu mpaka leo,
Mama Nyerere, amesema nimeamua kuyasema yote haya ili nisije nikasutwa na Baba wa taifa juu ya habari ya kwanini sijasema na kuwakanya watoto wa kizazi hiki ambacho kinajenga dhamira ya kutukana wazee wao kana kwamba wao ndio watukufu pekeee,
Amesema, Nchi kama ya misri ambayo imeingia katka machafuko imetokana na kushindwa kwa uongozi bora wa wananchi na hivyo kila mmoja kujiona bora kuliko mwenzake na mwisho wa siku Kuingia katika vita,
Ameniambia taifa hili kama halibadilika halina muda mrefu linaingia vitani, lazima ifike wakati watu wakajua kuwa kuingizwa umma vitani kunahsara yake tena ni hasara kubwa kuliko hiyo ambayo inawafanya mpaka wanatukuna waasisi wao,
Anasema nchi hii ni yetu na wakuharibu ni sisi, hivyo kuna kila sababu ya kuzuia vitendo vyote viavyoashria uvunjifu wa amani katika taifa hili, hasa hizi chokochoko za kutukana wazee wa taifa hili ambao walitumia ujana wao nguvu zao na ujuzi wao kulitumikia taifa hili,
Aidha katika hatua nyingine, Mama Maria Nyerere amewapongeza vijana wa CCM kwa kwenda kumpa pole kutokana na matusi alitukanwa mume wake huyo kipenzi na kusema ni vyema sasa wakazunguka hata Tanzania nzima kutangaza habari ya kutukanwa kwa wazee wetu kuwa si nzuri na badala yake tujikite katika namna ya kendeleza mazuri yote ambayo yamefanyika na kuongeza yale mazuri kwa maslahi ya taifa,.
No comments
Post a Comment